Datasets:
id
stringlengths 1
6
| url
stringlengths 31
202
| title
stringlengths 1
120
| text
stringlengths 8
182k
|
---|---|---|---|
2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Akiolojia | Akiolojia | Akiolojia (kutoka Kiyunani αρχαίος = zamani na λόγος = neno, usemi) ni somo linalohusu mabaki ya tamaduni za watu wa nyakati zilizopita. Wanaakiolojia wanatafuta vitu vilivyobaki, kwa mfano kwa kuchimba ardhi na kutafuta mabaki ya majengo, makaburi, silaha, vifaa, vyombo na mifupa ya watu.
Akiolojia na historia
Tofauti na somo la Historia, akiolojia haichunguzi sana maandishi hasa ili kupata ufafanuzi wa mambo ya kale. Historia inatazama zaidi habari zilizoandikwa lakini akiolojia inatazama vitu vilivyobaki kutoka zamani. Wanaakiolojia wanaweza kutumia maandishi na habari za historia wakiamua jinsi gani waendelee na utafiti wao, kwa mfano wachimbe wapi. Lakini hutumia mitindo ya sayansi mbalimbali kuchunguza vitu vinavyopatikana kwa njia ya akiolojia.
Kinyume chake, matokeo ya akiolojia ni chanzo muhimu kwa wachunguzi wa historia. Mara nyingi matokeo ya akiolojia yanaweza kupinga au kuthibitisha habari zilizoandikwa au kufungua macho kwa kuzielewa tofauti.
Mfano wa Pompei
Mfano bora wa akiolojia ni utafiti wa mji wa Pompei huko Italia. Habari za Pompei zimepatikana katika maandishi mbalimbali ya Kiroma, lakini mji uliharibika kabisa na kufunikwa na majivu ya volkeno Vesuvio mwaka 79 B.K.
Kuanzia mwaka 1748 wataalamu walianza kuchimba mahali pa mji mpotevu wakaupata. Hadi leo sehemu kubwa ya mji umefunuliwa tena. Chini ya majivu na udongo wa karne nyingi vitu vingi vimehifadhiwa vizuri ambavyo vingepotea kabisa visingefunikwa, kwa mfano picha za Kiroma zenye rangi nzuri kabisa kwenye kuta za nyumba. Hata mabaki ya chakula yamepatikana yakachunguzwa.
Afrika na akiolojia
Ujuzi wa akiolojia ni muhimu sana kwa ajili ya historia ya Afrika. Tamaduni nyingi za Afrika ziliendela bila maandishi hadi juzi au hata leo. Habari zetu kuhusu utamaduni wa Zimbabwe Kuu au kuhusu uenezi wa Wabantu hutegemea akiolojia kwa kiasi kikubwa sana.
Hivyo akiolojia huongeza ujuzi wetu kwa kufunua ushahidi wa nyakati za kale; wakati huohuo kazi ya akiolojia inahatarisha ushahidi huo kwa sababu kazi yake huondoa hifadhi ya udongo. Katika karne za kwanza za akiolojia mabaki mengi ya tamaduni za kale yameharibika kutokana na kufunuliwa kwao. Kuepukana na tatizo hilo ni jukumu muhimu la akiolojia ya kisasa.
Viungo vya nje
"The World Wide Web Library of African Archaeology
Sayansi
Historia |
10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Daktari | Daktari | Daktari (au dokta; wingi wake unaundwa kwa kutanguliza ma-) ni neno lenye asili ya Kilatini ("doctor") lililoingia Kiswahili kwa kupitia Kiingereza. Hutumiwa kwa maana mbili:
1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu cha kutibu maradhi ya wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu anaitwa pia mganga (wa), tabibu (ma). Daktari humtibu mgonjwa kwa kutumia sindano, kumtundikia dripu n.k. baada ya kumpima baadhi ya vitu kama:
Kumpima damu
Kumpima mapigo ya moyo n.k. Maranyingi daktari hufanya kazi yake katika sehemu maalumu iitwayo Hospitali.
2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu au "PhD" ambayo ni shahada ya juu kabisa.
Picha
Cheo
Elimu
Tiba |
16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia | Historia | Historia (kutoka Kigiriki ιστορια, historia; pia "tarehe" kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia": pia tena "mapisi") ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita.
Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").
Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake.
Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani.
Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (vita, uhuru, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi.
Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa historia ya awali).
Kurasa zinazohusiana
Historia ya Afrika
Historia ya Amerika
Historia ya Asia
Historia ya Australia
Historia ya Ulaya
Historia ya Wokovu
Historia ya Kanisa
Historia ya teolojia
Historia ya utawa
Historia ya Kanisa Katoliki
Historia ya Uislamu
Miaka
Vita
Tanbihi |
17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Historia%20ya%20Afrika | Historia ya Afrika | Historia ya Afrika ni historia ya bara hilo lililo asili ya binadamu wote.
Kwa ujumla, historia ni kumbukumbu ya maisha ya mwanadamu duniani, hasa ile tarehe iliyosajiliwa na kuhifadhiwa katika vitabu, maandishi mbalimbali, na simulizi au hekaya za mapokeo. Ingawa historia iliyobebwa katika simulizi na hekaya huchukuliwa na baadhi kuwa haina nguvu kwa kukosa ithbati ya maandishi, bado hivi ni vyanzo muhimu vya historia. Mara nyingi historia iliyoko katika maandishi huwa imehifadhiwa katika simulizi na hekaya kwa muda mrefu kabla ya kuandikwa.
Historia ya Afrika
Hapo kale, bara la Afrika lilishuhudia matukio mengi ya harakati za mwanadamu kuliko mabara mengine ya ulimwengu.
Wataalamu wa athari wamegundua athari za zamadamu zinazorudi nyuma kufikia hadi miaka milioni minne, na athari za ustaarabu wa Wamisri wa Kale huko Misri na Wafoinike huko Tunis na sehemu nyinginezo za Afrika ya Kaskazini katika karne ya 9 KK.
Harakati za madola makubwa ya Warumi na Waarabu ziliweza kuonekana kabla ya karne ya 4 BK, na Waarabu walianza kuingia Afrika huko Habasha (Ethiopia) tangu karne ya 7 BK na kutangaza dini ya Uislamu na kuieneza katika maeneo mbalimbali ya Afrika pamoja na kuanzisha biashara na ustaarabu na kuimarisha mamlaka zao katika Sudan ya wakati huo tangu karne ya 8 baada ya Kikristo.
Himaya za Ghana, Mali, na Songhai zilikuwa zikijulikana kwa utajiri mkubwa na biashara stawi iliyokuwa ikifanyika wakati huo ya dhahabu na bidhaa nyinginezo. Mwisho wa karne ya 15 BK, himaya ya Songhai ilikuwa na nguvu kuweza kuitia chini ya utawala wake mamlaka ya Mali. Sehemu nyingine za kusini mwa Afrika zilikuwa wakati huu hazijulikani sana, na historia yake ilikuwa bado haijasajiliwa.
Baina ya karne ya 1 KK na karne ya 16 BK watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kibantu watokao sehemu za Nigeria na Cameroon ya leo, ndio waliokuwa wameenea kwenye sehemu mbalimbali kusini mwa bara la Afrika, wakiwa wameanzisha vijiji, mashamba na mamlaka katika sehemu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya leo, za Luba na Mwememutapa, lakini makundi ya wachungaji wa wanyama walianza kuhamia kusini katika karne za 15 na 16 na kukutana na Wabantu. Ndipo walipoanzisha mamlaka zao za Bunyoro, Buganda, Rwanda na Ankole.
Ukoloni
Wazungu walianza kugundua bara la Afrika katika karne ya 15, wakati Wareno walipokuja kwenye fukwe za bara la Afrika kutafuta njia nyepesi na ya amani ya kufikia India, na kuweza kupata nafasi ya kushikilia biashara ya dhahabu na pembe na watumwa ambayo ilikuwa ikiendelea wakati huo katika bara la Afrika. Katika mwaka 1488 Bartolomeo Dias alizunguka Rasi ya Tumaini Jema (kwa Kiingereza: Cape of Good Hope), na katika mwaka 1498 Vasco da Gama alifika ufukwe wa Afrika Mashariki na kuendelea mpaka India.
Baada ya hapo, Ureno ulianzisha vituo vya biashara Afrika, ukifuatiwa na Waholanzi, Waingereza, Wafaransa na Wazungu wengineo, na biashara ya watumwa iliyosimamiwa na Waarabu na baadhi ya Waafrika wenyewe ikashika kani na kuwa na kasi na nguvu.
Wakati huohuo Waturuki walishikilia sehemu za kaskazini ya Afrika na Waomani wakashikilia ufukwe wa Afrika Mashariki.
Kati ya miaka 1880 na 1912, Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberia na Ethiopia.
Wafaransa wakachukuwa Afrika Magharibi na Kaskazini na kwa hivyo nchi za Afrika Magharibi: Dahomey (sasa Benin), Guinea, Mali, Cote d'Ivoire, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (sasa Burkina Faso) zilikuwa chini ya utawala wake. Hali kadhalika, Algeria, Tunisia na Morocco zilitawaliwa na wao. Aidha, Wafaransa walitawala Togoland, Somaliland, Madagascar, Comoro, na Reunion.
Waingereza nao wakatawala Afrika Mashariki na Kusini, na kuwa sehemu ya Sudan na Somalia, Uganda, Kenya, Tanzania (chini ya jina la Tanganyika), Zanzibar, Nyasaland, Rhodesia, Bechuanaland, Basutoland na Swaziland chini ya utawala wao na baada ya kushinda katika vita huko Afrika ya Kusini walitawala Transvaal, Orange Free State, Cape Colony na Natal, na huko Afrika ya Magharibi walitawala Gambia, Sierra Leone, the Gold Coast na Nigeria.
Wareno wakachukuwa sehemu ya Guinea, Angola na Msumbiji na sehemu na visiwa fulanifulani huko Afrika ya Magharibi.
Wabelgiji wakachukua Kongo na Rwanda-Urundi, na Wahispania wakachukua sehemu ya Guinea, Spanish Sahara (sasa Sahara ya Magharibi), Ifni na sehemu nyingine za Morocco.
Wajerumani nao wakachukua Togoland, Cameroon na baadhi ya nchi katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Mashariki, lakini baada ya vita vya kwanza vya dunia wakanyang'anywa.
Waitalia wakachukua Libya, Eritrea na sehemu kubwa ya Somalia.
Uhuru
Nchi ya kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910. Misri, katika mwaka wa 1922 walikuwa wanajiendesha wenyewe, na Tangier katika mwaka wa 1925.
Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960, na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru. Libya wakajinyakulia uhuru katika mwaka wa 1951, Eritrea katika mwaka 1952 ikiwa imejiunga na Ethiopia, Morocco katika mwaka wa 1956, na wakarudishiwa Tangier.
Katika mwaka huu wa 1956, Sudan na Tunisia vile vile walipata uhuru wao, na Ghana katika mwaka wa 1957, Guinea katika mwaka wa 1958, na vile vile Morocco wakarudishiwa Spanish Morocco.
Katika mwaka wa 1960 Ufaransa ukatoa uhuru kwa Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo (Brazzaville), Cote d'Ivoire, Dahomey (Benin), Gabon, Madagascar, Mali, Mauritania, Niger, Senegal na Volta ya Juu (Burkina Faso).
Vile vile, katika mwaka huohuo wa 1960 Congo (Kinshasa), Nigeria, Somalia, na Togo zikapata uhuru, na katika mwaka wa 1961 Sierra Leone na Tanganyika zikapata uhuru, na Afrika ya Kusini ikawa Jamhuri.
Katika mwaka wa 1962 Algeria, Burundi, Rwanda, na Uganda zikawa huru, na 1963 zikafuatia Zanzibar, Gambia na Kenya, na katika mwaka wa 1964 Malawi (Nyasaland), na Zambia (Rhodesia ya Kaskazini) zikapata uhuru.
Baada ya miaka miwili, katika mwaka wa 1966 Botswana (Bechuanaland) na Lesotho (Basutoland) zikajinyakulia uhuru. Mauritius na Swaziland katika mwaka wa 1968 na vile vile Guinea ya Ikweta. Hispania ikairudisha Ifni katika mwaka wa 1969 katika mamlaka ya Morocco.
Aidha, katika mwaka wa 1974 Guinea ya Kireno (Guinea-Bissau) ikapata uhuru wake, na katika mwaka wa 1975 Angola, Cape Verde, Mozambique, Sao Tome na Principe zikapata uhuru. Hispania vilevile ikaitoa Sahara ya Magharibi kwa Morocco na Mauritania katika mwaka wa 1976, lakini wananchi wakakataa kuwa chini ya nchi mbili hizi, kukazuka vita. Mauritania ukaitoa sehemu yake na kuipa Morocco katika mwaka wa 1979, tatizo ambalo mpaka sasa linaendelea baina ya Morocco na Sahara ya Magharibi, na Umoja wa Mataifa unajaribu kutatua tatizo hili. Waingereza wakawapa uhuru Shelisheli katika mwaka wa 1976, na Ufaransa ukatoa uhuru kwa visiwa vya Ngazija (Comoro).
Katika mwaka wa 1977 Jibuti (Nchi ya Afars na Issas) iliyokuwa ikitawaliwa na Wafaransa ikarudi kwa wenyewe. Rhodesia (Zimbabwe) ikapata uhuru halisi mwaka wa 1980, na South West Africa, iliyokuwa ikitawaliwa na Afrika ya Kusini ikapata uhuru katika mwaka 1990 na kuitwa Namibia.
Uingereza umebaki na visiwa vya Saint Helena na Ascension, na Ufaransa unaendelea kutawala Mayotte na Reunion. Hispania vilevile unaendelea kutawala visiwa vya Canarias pamoja na Ceuta na Melilla na visiwa viwili vingine vilivyoko karibu na Morocco.
Angalia pia
Historia Kuu ya Afrika (mradi wa UNESCO na vitabu)
Tanbihi
Marejeo
http://www.infoplease.com/ce6/world/A0856495.html
Korotayev A. & Khaltourina D. Introduction to Social Macrodynamics: Secular Cycles and Millennial Trends in Africa. Moscow: URSS, 2006. ISBN 5-484-00560-4 .
!
Afrika |
20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hesabu | Hesabu | Hesabu (afadhali: Hisabati kutoka neno la Kiarabu vilevile) ni somo linalohusika na idadi na jinsi tunavyoweza kuhesabu kwa kutumia hasa kanuni zifuatazo: kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawa n.k.
Hesabu ni sehemu ya msingi ya nadharia ya namba.
Hisabati |
24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Jiografia | Jiografia | Jiografia ni somo la Dunia na vipengele vyake, wakazi wake, na maajabu yake.
Neno la Kiswahili jiografia linafuata matamshi ya Kiingereza ya neno la Kigiriki "γεωγραφία", geo-grafia kutoka gê "dunia" na graphein "kuandika". Lina maana ya "kuandika kuhusu Dunia". Neno hili lilianza kutumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasayansi Eratosthenes (276-194 KK).
Sehemu za jiografia ni vitu kama mabara, bahari, mito na milima. Wakazi wake ni watu wote na wanyama waishio juu yake. Maajabu yake ni vitu vinavyotokea kama vile maji kujaa na kupwa, upepo, na tetemeko la ardhi.
Nchi za Afrika
Afrika ya Mashariki
Burundi
Eritrea
Jibuti
Kenya
Komoro
Rwanda
Shelisheli
Somalia
Tanzania
Uganda
Uhabeshi (Ethiopia)
Sudan Kusini
Afrika ya Kati
Gabon
Guinea ya Ikweta
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Jamhuri ya Kongo
Kamerun
Sao Tome na Principe
Afrika ya Kaskazini
Algeria
Libya
Misri
Moroko
Sahara ya Magharibi
Sudan
Tunisia
Afrika ya Kusini
Angola
Botswana
Eswatini
Lesotho
Malawi
Mauritius
Msumbiji (Mozambiki)
Namibia
Afrika Kusini
Zambia
Zimbabwe
Afrika ya Magharibi
Benin
Burkina Faso
Chadi
Cabo Verde
Ivory Coast
Gambia
Ghana
Guinea
Guinea Bisau
Liberia
Mali
Mauritania
Niger
Nigeria
Senegal
Sierra Leone
Togo
Nchi za Amerika ya Kaskazini
Kanada
Marekani (Maungano wa Madola ya Amerika)
Meksiko (Maungano a Madola ya Mexiko)
Nchi za Amerika ya Kati
Nchi za barani
Belize
Guatemala
Honduras
El Salvador
Nikaragua
Kosta Rika
Panama
*(Meksiko mara nyingi huhesabiwa katika Amerika ya Kati kwa sababu za kiutamaduni)
Nchi za visiwa vya Karibi
Antigua na Barbuda
Bahamas
Barbados
Dominica
Jamhuri ya Dominika
Grenada
Haiti
Jamaika
Kuba
Saint Kitts na Nevis
Saint Lucia
Saint Vincent na Grenadini
Nchi za Amerika ya Kusini
Argentina
Bolivia
Brazil
Chile
Ekuador
Guyana
Guyana ya Kifaransa
Kolombia
Paraguay
Peru
Surinam
Uruguay
Venezuela
Nchi za Asia
Asia ya Kati
Afghanistan
Kazakhstan
Kirgizistan
Mongolia
Tajikistan
Turkmenistan
Usbekistan
Asia ya Kaskazini
Siberia (sehemu ya Urusi)
Asia ya Mashariki
Uchina (pamoja na Taiwan)
Japani
Korea Kaskazini
Korea Kusini
Asia ya Kusini-Mashariki
Brunei
Indonesia
Kamboja
Laos
Malaysia
Myanmar (zamani iliitwa Burma)
Philippines
Singapur
Thailand (zamani iliitwa Siam)
Timor Mashariki
Vietnam
Asia ya Kusini
Bangladesh
Bhutan
Uhindi (au India)
Maledivi
Nepal
Pakistan
Sri Lanka (zamani iliitwa Ceylon)
Asia ya Magharibi
Armenia
Azerbaijan
Georgia
Irak
Israel
Yordani
Libanon
Palestina
Shamu (au: Syria)
Uajemi (au Iran au Persia)
Uturuki
Bara Arabu
Bahrain
Kuwait
Muungano wa Falme za Kiarabu
Oman
Qatar
Saudia
Yemen
Nchi za Ulaya
Nchi za Oceania
mfumo wa Jua
Jua
Utaridi
Zuhura (Ng'andu)
Dunia (Ardhi)
Mirihi (Meriki - Mars)
Mshtarii
Zohari
Uranus
Neptun
Tazama pia
Nchi
Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
Tanbihi
Viungo vya nje
Jiografia
Sayansi |
30 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiesperanto | Kiesperanto | Kiesperanto ni lugha ya kupangwa inayozungumzwa zaidi duniani kati ya lugha hizi. Ilipangwa na Ludwik Lejzer Zamenhof, myahudi aliyetoka mjini Białystok, nchini Urusi (siku hizi ni sehemu ya nchi ya Poland). Alitoa kitabu cha kwanza cha lugha hii mwaka 1887 baada ya kuitengeneza kwa miaka karibu kumi. Nia yake ilikuwa kutengeneza lugha rahisi ili iwe lugha saidizi ya kimataifa, lugha ya pili kwa kila mtu duniani. Waesperanto wengine bado wanataka hiyo, lakini wengine wanapenda kuitumia tu bila nia ya kuieneza duniani kote.
Waesperanto wanakitumia Kiesperanto kwa ajili ya kukutana na wageni na kujifunza kuhusu nchi na tamaduni nyingine. Siku hizi, maelfu ya watu wanaitumia mara kwa mara ili kuwasiliana na watu popote duniani.
Chunguzi za kitaalamu zimeonyesha kwamba Kiesperanto kinaweza kujifunzwa rahisi zaidi sana kuliko lugha asilia, na pia kwamba kujifunza Kiesperanto kwanza kunarahisisha kujifunza kwa lugha nyingine.
Sifa za kiisimu
Kwa kuwa lugha ya kupangwa, Kiesperanto hakiko katika familia yoyote a lugha. Maneno yake yanatoka hasa lugha za Kirumi (kama Kifaransa na Kilatini), lakini pia lugha za Kigermaniki (kama Kiingereza na Kijerumani) na lugha za Kislavoni (kama Kirusi na Kipolandi). Maneno mengi yanaumbwa kwa kuunganisha mzizi wa neno moja na viambishi au kwa kuunganisha mizizi ya maneno mbalimbali. Kwa mfano kuna kiambishi awali "mal-" inayoonyesha kinyume: "bona" ni "-zuri" na "malbona" ni "-baya". Kwa hiyo inawezekana kusema mambo mengi baada ya kujifunza maneno machache tu.
Matamshi na maandishi
Katika Kiesperanto kuna harufi 28 na kuna sauti 28. Kila harufi inaweza kutamka kwa sauti moja tu, na kila sauti inaandikwa kwa serufi moja tu. Harufi za Kiesperanto ni zifuatazo:
a b c ĉ d e f g ĝ h ĥ i j ĵ k l m n o p r s ŝ t u ŭ v z
Irabu zote (a, e, i, o, u) zinatamka kama kwa Kiswahili.
Kwa upande wa konsonanti, b, d, f, g, h, k, l, m, n, p, r, s, t, v na z zinatamka kama kwa Kiswahili. c inatamka kama ts. ĉ inatamka kama ch. Matamshi ya ĝ yanafanana na matamshi ya j kwa Kiswahili (ni sawasawa na matamshi ya j katika neno la Kiswahili "njia"); j ya Kiesperanto inatamka kama y ya Kiswahili. ĵ inatamka kama j ya Kifaransa (inafanana na sh ya Kiswahili, lakini inatamka na sauti, kama z). ŝ inatamka kama sh. ŭ inatamka kama w; ŭ inatumika baada ya a na e tu, ingawa Zamenhof wenyewe na Waesperanto wengine waiunganisha na irabu yoyote, k.m. "sŭahila" (Kiswahili), "ŭato" (wati), tena jina la herufi yenyewe ni "ŭo"; tofauti kati ya au na aŭ ni kwamba au inatamka kwa silabi mbili na aŭ kwa silabi moja.
Serufi
Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -oj (arboj = miti).
Vivumishi vinahitimu kwa kiambishi tawali -a, kwa mfano "alta" (-refu). Vivumishi kwa kawaida vinawekwa kabla ya nomino inayohusu, lakini pia inaweza kuwa baada yake. Wingi pia unaonyeshwa katika vivumishi kwa harufi "j": altaj arboj = miti mirefu.
Vitenzi vina viambishi tamati mbalimbali:
-i inatumika kwa vitenzi-jina (kwa mfano "fari" = "kufanya")
-as inatumika kwa njeo ya wakati uliopo (kwa mfano "mi faras" = "ninafanya"
-is inatumika kwa njeo ya wakati uliopita (kwa mfano "mi faris" = "nilifanya" au "nimefanya")
-os inatumika kwa njeo ya wakati ujao (kwa mfano "mi faros" = "nitafanya")
-us inatumika kwa hali a masharti (kwa mfano "mi farus" = "ningefanya")
-u inatumika kwa hali ya kuamuru (kwa mfano "faru!" = "fanya!"; "li faru" = "afanye")
Viungo vya nje
makala za OLAC kuhusu Kiesperanto
lugha ya Kiesperanto katika Glottolog
http://www.ethnologue.com/language/epo
Maelezo mengine kuhusu Kiesperanto
Jifunze Kiesperanto
Tangazo la Praha la jamii ya kiesperanto
TANGAZO LA PRAHA LA JAMII YA KIESPERANTO (Word-doc.)
esperanto-afriko.org
Jifunze lugha ya Kiesperanto, 2007,
Kozi ya kimataifa Kurso Saluton!
Lernu!
Lugha
Lugha saidizi ya kimataifa |
31 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20ya%20kuundwa | Lugha ya kuundwa | Lugha ya kuundwa (au lugha unde) ni lugha ambayo misamiati na sarufi zake zimetungwa na watu badala ya kukua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Kwa kawaida zinaundwa kwa ajili ya kuwasiliana kati ya watu sawasawa na lugha asilia. Nyingi zinatengenezwa ili kuwa lugha saidizi za kimataifa, lakini nyingine zinaundwa kwa ajili ya usiri au majaribio ya isimu au bila sababu fulani.
Lugha ya kuundwa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto.
Mara chache lugha ya kuundwa maana yake ni lugha za kompyuta au za kuandaa programu (angalia lugha asilia). Kwa sababu ya utata huo watu wengi, hasa Waesperanto, hawapendi kutumia neno lugha ya kuundwa, na badala yake wanasema lugha ya kupangwa. Msemo lugha ya kupangwa unatumika kwa lugha zile tu ambazo ziliundwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu, kama Kiesperanto.
Mfano mwingine wa lugha ya kuundwa ni lugha ya sheng' inayozungumzwa nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana. Lugha hiyo Haina wazawa asilia mahali popote ila tu ilizuka miongoni mwa vijana Kwa kutaka kusitiri mazungumzo Yao. Hivi ni kuunga mkono wazo la hapo awali kwamba lugha unde Huwa Kwa Sababu za kusitiri mazungumzo au kuunda programu za kompyuta kama vile lugha iitwaya "binary language" ambayo hutumika katika vifaa vya kielektroniki Ili kuundia programu zake. Lugha hiyo ndio hueleweka na mashine za kielektroniki kama tarakilishi au kikokotoo.
Marejeo
TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Massamba, David 2004 "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Lugha
Isimu |
32 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha | Lugha | Lugha (kutoka neno la Kiarabu: لغة) ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu (wengine wanadai hata kati ya viumbe wenye akili).
Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.
Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.
Maana ya neno "lugha"
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kuleta mawasiliano.
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu kwa sababu zilitokea kama bahati tu kwa binadamu. Wanyama hawatumii lugha kama chombo cha mawasiliano, kwa kuwa lugha ni sauti zenye maana na kukubaliwa na jamii.
Hakuna lugha bora zaidi duniani, kwa kuwa lugha zote zina ubora, mradi zikidhi matakwa ya jamii husika.
Mbali na maana ya kawaida kuna pia lugha ya ishara inayotumiwa na watu bubu. Katika fani ya programu za kompyuta ni kawaida kuongea juu ya "lugha ya kompyuta".
Umuhimu wa lugha
Lugha ni kitambulisho cha jamii
Lugha hutolea elimu
Lugha huleta mawasiliano katika jamii
Lugha hukuza utamaduni
lugha huburudisha
Tabia za lugha
Lugha huwa na tabia zifuatazo:
Lugha huzaliwa: ni kutokana na lugha nyingine moja au zaidi zilizotangulia kuwepo.
Lugha hukua: lugha hukua (kuongezeka kwa maneno, kuongezeka kwa idadi ya wazungumzaji, kuwa na mawanda mapana, kusanifiwa) kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii.
Lugha hutohoa: lugha ina tabia ya kuchukua au kukopa maneno kutoka lugha nyingine.
Lugha hufundishika: mtu yeyote anaweza kujifunza walau kiasi lugha yoyote hata kwa njia ya ufundishaji.
Lugha huathiriana: lugha yoyote inaweza kuathiriwa na lugha nyingine.
Lugha lazima ijitosheleze: kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii inayotumia lugha yenyewe.
Lugha zina ubora: lugha zote ni bora hakuna lugha bora kuliko nyingine zote.
Lugha hurithiwa: jamii hurithi lugha kutoka kizazi hadi kizazi.
Lugha hufa: inapozidi mno kubadilika mwisho si yenyewe tena, lakini pia inapoachwa isitumike tena kwa kuwa wahusika wanapendelea lugha nyingine.
Sifa za lugha
Lugha lazima iwe inahusu binadamu
Sauti-sauti hufanywa na mwanadamu
Lugha hufuata misingi ya fonimu, yaani, a, b, ch, d, f, h, z n.k.
Lugha huwa na mpangilio maalumu wenye kubeba maana. Mpangilio huo huanza na fonimu ---> Silabi ---> Neno
Lugha hujitambulisha ili kuzalisha maneno mengi.
Dhima za lugha
Lugha hutumika kama chombo cha mawasiliano kwa kupashiana habari.
Lugha hutumika kujenga umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wanajamii.
Lugha hutumika kutunza, kukuza, na kuendeleza utamaduni wa jamii.
Lugha hutumika katika kutetea maarifa mbalimbali (ni nyenzo ya kufundishia).
Lugha hutumika kama alama ya utambulisho wa kabila/jamii au taifa fulani.
lugha hutumika kutoa burudani.
Aina za lugha kwa kigezo cha uwasilishaji
Kimsingi lugha ni moja. Uwasilishwaji wake ndio huigawa katika tanzu/aina kuu mbili:
Lugha ya mazungumzo
Lugha ya maandishi
Lugha ya mazungumzo
Hii ni lugha ambayo huwasilishwa na watu kwa njia ya mazungumzo ya mdomo - na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mazungumzo. Lugha ya mazungumzo ni kongwe, hai na halisi zaidi ya mzungumzaji na ina maana nyingi, kwani mzungumzaji na msikilizaji huwa ana kwa ana katika mazingira mamoja.
Stadi za lugha ya mazungumzo ni kuzungumza na kusikiliza.
Lugha ya maandishi
Hii ni lugha ambayo huwasilishwa kwa njia ya maandishi. Hii ni kiwakilishi cha lugha ya mazungumzo katika mfumo wa maandishi. Lugha ya maandishi ni changa kwani imeanza milenia za hivi karibuni baada ya kuvumbuliwa kwa maandishi.
Stadi za lugha ya maandishi ni kuandika na kusoma:
Kwa kawaida, lugha ni sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Lugha ya aina hii inaitwa lugha asilia. Lakini pia kuna lugha za kuundwa.
Nyanja za lugha
Lugha ina nyanja kuu mbili, nazo ni:
Sarufi - hushughulikia kanuni za lugha
Fasihi - hushughulikia sanaa zitokanazo na lugha husika ili kuumba kazi mbalimbali za kifasihi.
Kukua na kufa kwa lugha
Tangu siku za kwanza za binadamu, lugha zimekuwa zikichipuka, kukua, kutangaa na kufa kama kiumbe yeyote mwingine. Kwa hivyo, lugha zilizopo leo ulimwenguni, huenda baada ya karne nyingi kupita zikatoweka na kuzuka nyinginezo.
Leo ulimwenguni mathalan, kuna lugha karibu 6,700, zikiwa 1,000 katika bara la kaskazini na la kusini la Amerika, 2,000 zikiwa kwenye bara la Afrika, 230 katika bara la Ulaya, 2,200 katika bara la Asia, na 1,300 katika bara la Oshania (Australia na nchi jirani nayo).
Kurasa zinazohusiana
Lugha asilia
Lugha ya kuundwa
Lugha mama
Lugha ya pili
Tazama pia
Lango la lugha
Viungo vya nje |
33 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20asilia | Lugha asilia | Lugha asilia ni lugha ambayo ilikua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani ambao watu wake wanaiongea kama lugha mama. Ni kinyume cha lugha ya kuundwa (lughaundwe).
Mara nyingine lugha asilia maana yake ni lugha yoyote ambayo inaweza kuzungumzwa na watu, huku lugha za kompyuta na za kuandaa programu zinaitwa lugha za kuundwa.
Mara nyingine tena lugha asilia ni lugha ambayo mtu huzaliwa nayo au huikuta baada ya kuzaliwa. Hata hivyo lugha asilia huwa chimbuko la watu fulani katika jamii na hutofautisha jamii moja na nyingine. Mara nyingi ni sehemu ndogo tu ya jamii ndiyo huwa na lugha asilia yaani kila ukoo au kabila huwa na lugha yake ya asili.
Lugha |
65 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Madola | Madola | Katika mabara, lile lenye nchi nyingi zaidi ni Afrika likiwa na nchi au madola 54, likifuatiwa na bara la Ulaya likiwa na madola 48, kisha Asia likiwa na madola 44, halafu Amerika ya Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati likiwa na madola 23, na baada yake ni Australia na Pasifiki (Oshania) likiwa na madola 14, na mwishowe ni Amerika ya Kusini likiwa na madola 12. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 195 ulimwenguni.
Nchi za Ulimwengu
(AS)= Asia (AF)= Afrika (NA)= Amerika ya kaskazini (SA)= Amerika ya kusini (A)= Antaktika (EU)= Ulaya na (AU)= Australia na nchi za Pasifiki.
(A)
Afghanistan (Kabul) (AS)
Afrika Kusini (Pretoria, Cape Town, Bloemfontein) (AF)
Albania (Tirana) (EU)
Algeria (Algiers) (AF)
Andorra (Andorra la Vella) (EU)
Angola (Luanda) (AF)
Antigua na Barbuda (St. John's) (NA)
Argentina (Buenos Aires) (SA)
Armenia (Yerevan) (EU)
Australia (Canberra) (AU)
Austria (Vienna) (EU)
Azerbaijan (Baku) (AS)
(B)
Bahamas (Nassau) (NA)
Bahrain (Manama) (AS)
Bangladesh (Dhaka) (AS)
Barbados (Bridgetown) (NA)
Belarus (Minsk) (EU)
Belize (Belmopan) (NA)
Benin (Porto Novo) (AF)
Bhutan (Thimphu) (AS)
Bolivia (Sucre) (SA)
Bosnia na Herzegovina (Sarajevo) (EU)
Botswana (Gaborone) (AF)
Brazil (Brasilia) (SA)
Brunei (Bander Seri Begawan) (AS)
Bulgaria (Sofia) (EU)
Burkina Faso (Ouagadougou) (AF)
Burma/Myanmar (Yangon) (AS)
Burundi (Bujumbura) (AF)
(C)
Cabo Verde (Praia) (Ureno)
Cambodia (Phnom Penh) (AS)
Chad (N'Djamena) (AF)
Chile (Santiago de Chile) (SA)
Colombia (Bogota) (SA)
Costa Rica (San Jose) (NA)
Cote d'Ivoire/Ivory Coast (Yamoussoukro) (AF)
Cuba (Havana) (NA)
(D)
Denmark (Copenhagen) (EU)
Djibouti (Djibouti) (AF)
Dominica (Roseau) (NA)
Dominican Republic (Santo Domingo) (NA)
(E)
Eire (Dublin) (EU)
Ekuador (Quito) (SA)
El Salvador (San Salvador) (NA)
Eritrea (Asmara) (AF)
Estonia (Tallinn) (EU)
Eswatini (Mbabane) (AF)
Ethiopia (Addis Ababa) (AF)
(F)
Falme za Kiarabu (Abu Dhabi) (AS)
Fiji (Suva) (Australia na Pasifiki)
(G)
Gabon (Libreville) (AF)
Gambia (Banjul) (AF)
Georgia (Tbilisi) (EU)
Ghana (Accra) (AF)
Grenada (St. George's) (NA)
Guatemala (Guatemala City) (NA)
Guinea (Conakry) (AF)
Guinea-Bisau (Bisau) (AF)
Guinea ya Ikweta (Malabo) (AF)
Guyana (Georgetown) (SA)
(H)
Haiti (Port-au-Prince) (NA)
Hispania (Madrid) (EU)
Honduras (Tegucigalpa) (NA)
Hungaria (Budapest) (EU)
(I)
Iceland (Reykjavik) (EU)
Indonesia (Jakarta) (AS)
Iraq (Baghdad) (AS)
Israel (Jerusalem) (AS)
Italia (Roma) (EU)
(J)
Jamaika (Kingston) (NA)
Jamhuri ya Afrika ya Kati (Bangui) (AF)
Japani (Tokyo) (AS)
(K)
Kamerun (Yaounde) (AF)
Kanada (Ottawa) (NA)
Kazakstan (Astana) (AS)
Kenya (Nairobi) (AF)
Kirgizia (Bishkek) (AS)
Kiribati (Teinainano) (AU - Oceania)
Komoro (Moroni) (AF)
Kongo (Jamhuri ya) (Brazzaville) (AF)
Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) (Kinshasa) (AF)
Korea, Kaskazini (Pyonyang) (AS)
Korea, Kusini (Seoul) (AS)
Kroatia (Zagreb) (EU)
Kupro (Nicosia) (AS) and/or (EU)
Kuwait (Kuwait City) (AS)
(L)
Laos (Vientiane) (AS)
Latvia (Riga) (EU)
Lebanon (Beirut) (AS)
Lesoto (Maseru) (AF)
Liberia (Monrovia) (AF)
Libya (Tripoli) (AF)
Liechtenstein (Vaduz) (EU)
Lithuania (Vilnius) (EU)
Luxemburg (Luxemburg) (EU)
(M)
Madagascar (Antananarivo) (AF)
Malawi (Lilongwe) (AF)
Malaysia (Kuala Lumpur) (AS)
Maldives (Male) (AS)
Mali (Bamako) (AF)
Malta (Valletta) (EU)
Marekani (Washington D.C.) (NA)
Marshall Islands (Majuro) (AU - Oceania)
Masedonia Kaskazini (Skopje) (EU)
Mauritania (Nouakchott) (AF)
Mexiko (Mexico City) (NA)
Micronesia (Palikir) (AU - Oceania)
Misri (Cairo) (AF)
Moldova (Chisinau) (EU)
Monaco (Monaco) (EU)
Mongolia (Ulan Bator) (AS)
Morisi (Port Louis) (AF)
Moroko (Rabat) (AF)
Montenegro (Podgorica) (EU)
Msumbiji (Maputo) (AF)
(N)
Namibia (Windhoek) (AF)
Nauru (Yaren)) (AU - Oceania)
Nepal (Kathmandu) (AS)
Nicaragua (Managua) (NA)
Niger (Niamey) (AF)
Nigeria (Abuja) (AF)
Norwei (Oslo) (EU)
New Zealand (Wellington) (AU)
(O)
Oman (Muscat) (AS)
(P)
Pakistan (Islamabad) (AS)
Palau (Melekeok) (AU - Oceania)
Panama (Panama City) (NA)
Papua Nyugini (Port Moresby) (AU)
Paraguay (Asuncion) (SA)
Peru (Lima) (SA)
Poland (Warsaw) (EU)
(Q)
Qatar (Doha) (AS)
(R)
Romania (Bucharest) (EU)
Rwanda (Kigali) (AF)
(S)
Sahara ya Magharibi (AF)
Saint Kitts na Nevis (Basseterre) (NA)
Saint Lucia (Castries) (NA)
Saint Vincent na Grenadini (Kingstown) (NA)
Samoa (Apia) (AU - Oceania)
San Marino (San Marino) (EU)
Sao Tome na Principe (Sao Tome) (AF)
Saudia (Riyadh) (AS)
Senegal (Dakar) (AF)
Serbia (Belgrad) (EU)
Shelisheli (Victoria (Shelisheli)) (AF)
Sierra Leone (Freetown) (AF)
Singapuri (Jiji la Singapuri) (AS)
Slovakia (Bratislava) (EU)
Slovenia (Ljubljana) (EU)
Solomon Islands (Honiara) (AU - Oceania)
Somalia (Mogadishu) (AF)
Sri Lanka (Sri Jayawardenapura) (AS)
Sudan (Khartoum) (AF)
Sudan Kusini (Juba) (AF)
Suriname (Paramaribo) (SA)
Syria (Damascus) (AS)
(T)
Taiwan (Taipei) (AS)
Tajikistan (Dushanbe) (AS)
Tanzania (Dodoma) (AF)
Timor ya Mashariki (Dili) (AS)
Togo (Lome) (AF)
Tonga (Nuku'alofa) (AU - Oceania)
Trinidad na Tobago (Port of Spain) (NA)
Tunisia (Tunis) (AF)
Turkmenistan (Ashgabat) (AS)
Tuvalu (Funafuti) (AU - Oceania)
(U)
Uajemi (Tehran) (AS)
Ubelgiji (Brussels) (EU)
Ucheki (Prague) (EU)
Uchina (Beijing) (AS)
Ufaransa (Paris) (EU)
Ufilipino (Manila) (AS)
Ufini (Helsinki) (EU)
Uganda (Kampala) (AF)
Ugiriki (Athens) (EU)
Uhindi (New Delhi) (AS)
Uholanzi (Amsterdam, Den Haag) (EU)
Uingereza (London) (EU)
Ujerumani (Berlin) (EU)
Ukraine (Kiev) (EU)
Ureno (Lisbon) (EU)
Uruguay (Montevideo) (SA)
Urusi (Moscow) (EU, AS)
Uswidi (Stockholm) (EU)
Uswisi (Bern) (EU)
Uthai (Bangkok) (AS)
Uturuki (Ankara) (AS) & (EU)
Uzbekistan (Tashkent) (AS)
(V)
Vanuatu (Port Vila) (AU - Oceania)
Vatikani (EU)
Venezuela (Caracas) (SA)
Vietnam (Hanoi) (AS)
(Y)
Yemen (Sana'a) (AS)
Yordani (Amman) (AS)
(Z)
Zambia (Lusaka) (AF)
Zimbabwe (Harare) (AF)
Tazama pia
Orodha ya nchi kufuatana na wakazi
Marejeo
http://www.infoplease.com
http://www.worldatlas.com
Yale Africa Guide Interactive - Nations of Africa
Nchi
Orodha za kijiografia
nds:Land#Länner
sv:Världsgeografi#Lista över länder |
71 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Sayansi | Sayansi | Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.
Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.
Aina za sayansi
Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:
Sayansi Asili k.m.
Biolojia
Jiografia
Zoolojia
Sayansi Umbile k.m.
Fizikia
Hisabati
Kemia
Sayansi Jamii k.m.
Historia
Elimu
Saikolojia
Siasa
Sayansi Tumizi k.m.
Teknolojia
Uhandisi
Pia, kuna sayansi zinazohusu mada maalumu mbalimbali:
Maarifa
Astronomia
Tiba
Mbinu za kisayansi
Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli fulani.
Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka toka nadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitia majaribio rasmi, hutengeneza dhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo na tabia.
Hivyo, asili ya njia ya kisayansi ni mtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamo wanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Zisipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiri ukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.
Sura ya kisayansi
Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia ya atomu inasema kwamba katika jiwe (maada yabisi) kuna uvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha na maada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.
Historia
Sura ya kiutamaduni
Sayansi iliaanza kama udadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyo jumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali.
Hii hufanya mkururo wa ugunduzi ama uvumbuzi kuwa sehemu ya historia ya sayansi. Majina na sifa hutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.
Sayansi na jamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.
Sayansi na siasa za dunia
Katika dunia hii ya leo, maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.
Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ni nguvu inayoweza kubadili maisha ya watu kwa wema; lakini katika kilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu za mamlaka na fedha hushikilia baadhi ya matunda yake katika hali ya kibiashara na kiutawala zaidi.
Sayansi na maendeleo
Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tu mikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.
Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.
Tazama pia
Mtu wa kwanza alitoka wapi
Tanbihi
Sayansi |
72 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Sheria | Sheria | Sheria (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza law ) ni mfumo wa kanuni, ambazo kwa kawaida hutekelezwa kupitia seti ya taasisi maalumu. Inaunda siasa, uchumi na jamii kwa njia mbalimbali na huratibu mahusiano baina ya watu.
Sheria ya mkataba huongoza kila kitu, kuanzia kununua tiketi ya basi hadi biashara katika masoko.
Sheria ya mali inafafanua haki na wajibu unaohusiana na uhamisho wa jina la mali ya binafsi na mali ya kweli.
Sheria ya hifadhi inatumika kwa mali yanayotumika kwa uwekezaji na usalama wa kifedha, huku sheria ya kukiuka wajibu inaruhusu madai ya fidia ikiwa haki au mali za mtu zinafanyiwa madhara.
Ikiwa madhara ni kinyume cha sheria, sheria ya jinai inatoa mbinu zinazoweza kutumiwa na taifa ili kumshtaki mhusika.
Sheria ya kikatiba inatoa utaratibu wa utungaji wa sheria, ulinzi wa haki za kibinadamu na uchaguzi wa wawakilishi wa kisiasa.
Sheria ya utawala inatumika kuangalia upya maamuzi ya vyombo vya serikali, huku sheria ya kimataifa inatawala shughuli baina ya nchi huru zinazohusu mambo kama vile biashara, vikwazo vya kimazingira na hatua za kijeshi.
Akiandika mnamo 350 K.K., mwanafalsafa wa Ugiriki ya Kale Aristotle alisema, "Utawala wa sheria ni bora kuliko utawala wa mtu yeyote binafsi."
Mifumo ya sheria inaelezea haki na majukumu kwa njia mbalimbali. Tofauti ya jumla inaweza kufanywa kati ya maeneo yanayotawaliwa na mfumo wa sheria ya kiraia, ambayo huandika sheria zao, na yale yanayofuata sheria za kawaida, ambapo sheria haijaundwa kwa utaratibu maalumu. Katika baadhi ya nchi, sheria ya dini bado hutumika kama sheria maalum. Sheria ni chanzo kikuu cha uchunguzi wa kitaalam, wa historia ya sheria, falsafa ya sheria, uchambuzi wa kiuchumi wa sheria au somo la kijamii kuhusu sheria.
Sheria pia huibua masuala muhimu na magumu kuhusu usawa, uadilifu na haki. "Katika usawa wake wa ajabu", alisema mwandishi Anatole France mnamo mwaka 1894, "sheria inakataza matajiri na mafukura kulala chini ya madaraja, kuombaomba barabarani na kuiba mikate." Katika demokrasia ya kawaida, taasisi za msingi za kutafsiri na kuunda sheria ni matawi matatu makuu ya utawala, ambayo ni mahakama isiyo na upendeleo, bunge na serikali yenye kuwajibika.
Ili kutekeleza na kutumia nguvu za kufanya sheria ifuatwe na kutoa huduma kwa umma, urasimu wa serikali, jeshi na polisi ni muhimu. Vyombo hivyo vyote vya dola viliundwa na kutawaliwa na sheria, taaluma ya kisheria iliyo huru na jamii yenye bidii zinajulisha na kusaidia maendeleo.
Masomo ya sheria
Mifumo yote ya kisheria inahusu na masuala ya msingi, lakini kila taifa inaainisha na kubainisha masomo yake ya kisheria kwa njia mbalimbali. Tofauti ya kawaida ni kuwa "sheria ya umma" (maneno yanayohusika kwa karibu na taifa, na kuhusisha sheria ya kikatiba, kitawala na ya jinai), na "sheria ya kibinafsi" (inayohusisha mkataba, sheria ya kukiuka wajibu na mali). Katikamifumo ya sheria ya kirai , mkataba na kukiuka wajibu zinapatikana chini ya sheria ya majukumu huku sheria ya hifadhi inapatikana chini ya serkali za halali au mikataba ya kimataifa. Sheria ya Kimataifa, kikatiba, kitawala, jinai, mkataba, kukiuka wajibu na mali na hifadhi zinatambulika kama "masomo msingi ya jadi", ingawa kuna masomo zaidi ambayo yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa zaidi wa kiutendaji.
Sheria ya Kimataifa
Sheria ya kimataifa inaweza kuashiria mambo matatu: sheria ya umma ya kimataifa, sheria ya kibinafsi ya kimataifa au mgongano wa sheria na sheria ya mashirika makubwa ya kimataifa.
Sheria ya Umma ya Kimataifa inajihusisha na uhusiano kati ya mataifa uhuru. Vyanzo vya maendeleo ya sheria ya umma ya kimataifa ni desturi, mwenendo na mikataba kati ya nchi huru Mikataba ya Geneva. Sheria ya umma ya kimataifa inaweza kutengezwa na mashirika ya kimataifa, kama vile Umoja wa Mataifa (ambao ilianzishwa baada ya kushindwa kwa Shirikisho la Kimataifa kuzuia Vita vya Vikuu vya Pili vya Dunia), Shirika la Kimataifa la Ajira, Shirika la Kimataifa la Biashara, au Shirika la Fedha la Kimataifa. Sheria ya kimatifa ya umma ina hadhi maalum kama sheria kwa sababu hakuna kikozi cha kimataifa cha polisi, na mahakama (kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Haki kama tawi la kimsingi la Umoja wa Mataifa la mahakama) halina uwezo wa kuadhibu kutokutii. Hata hivyo, miili michache, kama vile WTO, ina mifumo yenye ufanisi ya utatuzi wa kudumu na utatuzi wa mogogoro inayoambatana na vikwazo vya kibiashara.
Mgongano wa sheria (au "sheria ya kibinafsi ya kimataifa" katika nchi za sheria ya kiraia) unahusisha maeneo ya kimamlaka ya kisheria ya mgogoro wa kisheria baina ya watu wa kibinafsi unafaa kusikizwa na sheria za maeneo gani ya kimamlaka ya kisheria ndiyo inayofaa kutumika. Leo, biashra zinazidi kuwa na uwezo wa kusongeza minyororo ya ugavi ya mtaji na ajira kuvuka mipaka, na pia kufanya biashara na kampuni za nchi za ng'ambo, hivyo kulifanya swali kuhusu nchi ipi ndiyo inayomamlaka ya kisheria kuwa muhimu zaidi. Idadi kubwa zaidi ya biashara zinachagua usuluhishi wa kibiashara chini ya Mkataba wa New York wa mnamo mwaka1958.
Sheria ya Umoja wa Ulaya ndiyo ya kwanza, kufikia sasa, ambayo ni mfano wa sheria kuu ya kimataifa. Kutokana na mwenendo wa kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi Duniani, mikataba mingi ya kikanda — hasa ya Umoja wa Nchi za Amerika Kusini — zimeanza kuufuata mfano kama huu. Katika Umoja wa Ulaya, nchi huru zimekusanya mamlaka yao katika mfumo wa mahakama na taasisi za kisiasa. Taasisi hizi zinapewa uwezo wa kutekeleza kanuni za kisheria dhidi ya au kwa nchi wanachama na raia katika namna ambayo haiwezekani kupitia sheria ya umma ya kimataifa. Kama Mahakama ya Ulaya ya Haki yalivyosema katika miaka ya 1960, sheria ya Umoja wa Umoja wa Ulaya hujumiusha "muundo mpya wa sheria ya kimataifa" kwa ajili ya faida inayotegemeana ya kijamii na kiuchumi wa nchi zote wanachama.
Sheria ya kikatiba na ya kiutawala
Sheria ya kikatiba na kiutawala zinasimamia mambo ya nchi. Sheria ya kikatiba inahusisha uhusiano baina ya serikali, bunge na mahakama na haki za kibinadamu au uhuru wa kiraia wa watu binafsi dhidi ya nchi. Maeneo mengi ya kisheria, kama vile Marekani na Ufaransa, zina katiba moja iliyoandikwa kwa makini, iliyo na Muswada wa Haki. Katiba chache kama vile Uingereza, hazina hati kama hiyo."Katiba" kwa ufupi ni zile sheria ambazo zinajumuisha mwili wa kisiasa, kutoka kanuni, sheria za uamuzi na mkataba. Kesi kwa jina Entick dhidi ya Carrington ilionyesha wazi kanuni ya kikatiba inayotokana na sheria ya kawaifa. Nyumba ya Bwana Entick ilifanyiwa upekekuzi na Afisa mmoja wa polisi aliyeitwa Carrington. Wakati Bwana Entick alipolalamika mbele ya mahakama, Afisa Carrington alidokeza kwamba kibali kutoka waziri wa Serikali, Ali wa Halifax, kilikuwa na mamlaka halali. Hata hivyo, hakukuwa na sheria iliyoandikwa au mamlaka ya kimahakama ambayo yalitoa uwezo huo.Hakimu mkuu, Bwana Camden, alisema,
Mwisho mkubwa, ambao ulifanya watu kuingia katika jamii, ilikuwa kupata mali. Haki hiyo imetunzwa na ni takatifu na haiwezi kuondolewa wakati wowote, ambapo haijaondolewa au kufupishwa na sheria fulani ya umma kwa manufaa ya wote...Hakuna sababau inayoweza kupatikana au kutolewa, kimya cha vitabu ni mamlaka dhidi ya mshtakiwa, na aliyeathiriwa lazima atendewe haki.
Kanuni ya kimsingi ya kikatiba, ilitokana na John Locke, inadokeza ya kwamba mtu binafsi anaweza kufanya isipokuwa kile ambacho kimekataliwa kisheria. Sheria ya utawala ndiyo mbinu msingi ya kufanya mashirika ya umma yawajibike. Watu wanaweza kutumia mapitio ya kimahakama kwa matendo au uamuzi uliofanywa na za halmashauri za mitaa, huduma za umma au wizara za serikali, kuhakikisha kuwa zinazingatia sheria. Mahakama ya kwanza ya maalum ya kiutawala yalikuwa mahakama ya Conseil d'État yaliyoundwa mnamo mwaka wa 1799, wakati Napoleon Bonaparte alipochukua mamlaka nchini Ufaransa.
Sheria ya jinai
Sheria ya jinai, inayojulikana pia kama sheria ya kuadhibu, inahusisha makosa na adhabu. Kwa hivyo inapima ufafanuzi wa adhabu ya makosa yaliyopatikana kuwa na madhara yanaonekana kuwa na uwezo wa kusababisha uharibifu lakini, kwa undani, haifanyi uamuzi wa kimaadili kumhusu mkosaji wala kuwekea jamii vikwazo ambavyo vinakataza watu kimwili wasifanye makoa mwanzoni. Investigating, apprehending, charging, and trying suspected offenders is regulated by the law of criminal procedure. Kesi ya kidhana ya uhalifu inatokana na ushahidi, kuzidi shaka ya kuridhisha, kuwa mtu ana hatia ya mambo mawili. Kwanza, mshtakiwa lazima awe amefanya kitendo ambacho kinatazamwa na jamii kuwa hatia, au actus reus (kitendo cha hatia). Pili, lazima mshtakiwa awe na dhamira ya kufanya uharibifu ya kufanya kitendoo fulani cha jinai, au mens rea (akili ya hatia). Hata hivyo, kwa kile kinachojulikana kama hatia za "dhima kali", actus reus haitoshi. Mifumo ya jinai ya utamaduni wa sheria ya raia zinatofautisha kati ya nia katika dhana pana (dolus directus na dolus eventualis), na uzembe. Uzembe hauna jukumu la jinai isipokuwa ambapo hatia fulani una adhabu yake maalum.
Mifano ya uhalifu ni mauaji, kushambulia, udanganyifu na wizi. Katika mifano maalum utetezi unaweza kutumika kwa vitendo maalum, kama zile kuuwa ili utetezi wa kibinafasi, au katika nyakati maalum kujitetea kuwa wazimu. Mfano mwingine ni katika kesi ya karne ya 19 ya Jamhuri dhidi ya Dudley na Stephens, iliyopima utetezi wa "kimahitaji". Meli ya Mignonette, iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Southampton kuelekea mji wa Sydney, ilizama. Wafanyikazi watatu wa meli hiyo na Richard Parker, kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17, walibaki katika meli iliyoundwa na vijiti. Walikuwa na njaa na kijana yule alikuwa karibu kufa. Kwa sababu ya kuwa na njaa iliyokithiri, wafanyikazi hao walimuuwa kijana yule na kumla. Wafanyikazi hao waliokolewa, lakini wakafikishwa mahakamani huku wakiwa na hatia ya mauaji. Walijitetea kwa kusema kwamba ilihitajika kwa lazima kwa wao kumuuwa kijana yule ili kuyaokoa maisha yao. Bwana Coleridge, akieleza kukataa kukubwa, aliamua, "kuhifadhi maisha ya kibinafsi ni, kwa kuzungumza kijumla, wajibu, lakini inaweza kuwa jukumu kuu kuyatoa maisha hayo kama kafara." Wanaume hao walihukumiwa nyonga, lakini maoni ya umma uliunga mkono haki ya wafanyikazi wale wa meli kuyaokoa maisha yao. Mwishowe, Ufalme ulipunguza hukumu zao hadi miezi sita gerezani.
Makosa ya jinai yanatambulika si tu kama makosa dhidi ya waathirika binafsi, lakini jamii pia. Taifa, kawaida likisaidiwa na polisi, huongoza mashitaka, basi hiyo ndiyo sababu mbona katika nchi zenye sheria ya kawaida kesi hutajwa kama "Watu dhidi ya..." au "Jamhuri (kwa "Rex" au Regina) dhidi ya..." Pia, jopo la waamuzi ambao hutokana na raia wa kawaida hutumika kuamua hatia ya washitakiwa kutokna na pointi zinazoweza kubainika ukweli: jopo la waamuzi haliwezi kubadilisha kanuni za kisheria. Baadhi ya nchi zilizostawi bado hutumia adhabu ya kifo kwa matendo ya jinai lakini adhabu ya kawaida ya uhalifu itakuwa ni kufungwa gereza, faini usimamizi wa taifa (kama vile probesheni), au huduma ya kijamii. Sheria ya kisasa ya jinai imeathiriwa vilivyo na sayansi ya jamii, hasa kuhusu kuhukumu, utafiti wa kisheria, kuunda sheria, na kuwasaidia wahalifu kurekesha mwenedo wao. Katika ngazi ya kimataifa, nchi 108 wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ambayo ilianzishwa kuwahukumu watu kwa hatia dhidi ya ubinadamu.
Sheria ya mkataba
Sheria ya mkataba inahusu ahadi zinazowezwa kutendwa, na inaweza kuandikwa kwa ufupi katika maneno ya Kilatinipacta sunt servanda (ahadi lazima zitimizwe). Katika maeneo ya kimamlaka ya sheria ya kawaida, vipengele vitatu muhimu kuhusu utengenezaji wa mkataba vinahitajika: kutoa na kukubali, kutilia maanani na nia ya kutengeneza uhusiano wa kisheria.Katika kesi ya Carlill shisi ya Kampuni ya Carbolic Smoke Ball kampuni ya matibabu ilitangaza kuwa dawa yake mpya ya ajabu, smokeball, ingewatibu watu kutokana na mafua, na ikiwa haingefaulu kuwatibu, wanunuzi wangepata £ 100. Watu wengi waliwasilisha kesi mahakamani ili wapate £100 zao wakati dawa hiyo iliposhindwa kuwatibu. Ikiogopa kufilisika, Kampuni ya Carbolic ilijitetea kwa kusema kuwa tangazo lile lilikuwa mzaha tu, na kwa hivyo halikuwa toleo lenye nguvu za kisheria. Lilikuwa karibisho, mchezo tu. Lakini mahakama ya rufaa yaliamua kuwa kwa mtu mwenye kufikiria kwa kawaida kampuni ya Carbolic ilikuwa imefanya toleo. Watu walikuwa wametoa kusudi la kununua bidhaa ile kwa kupitia "shida bayana" ya kutumia bidhaa yenye hitilafu. "Soma tangazo vile utakavyo, na ulibadilishe tangazo hilo vile utakavyo", alisema Hakimu Lindley, "haa kuna ahadi maalum ilitajwa katika lugha isyokuwa na utata wowote".
"Kutilia maanani" knaonyesha ukweli kwamba vyama vyote katika mkataba vimebadilisha kitu fulani chenye maana. Baadhi ya mifumo ya sheria ya kawaida, ikiwemo Australi, zinasonga mbali kutoka dhana ya kutilia maanani kama mojawapo ya mahitaji ya mkataba. Dhana ya "estoppel" au culpa in contrahendo, inaweza kutumika kuunda wajibu wakati mazungumzo kabla ya kuingia mkataba Katika maeneo ya kisheria ya kiraia, kutilia maanani si lazima kwa mkataba kuwa na nguvu ya kisheria. Nchini Ufaransa, mkataba wa kawaida unasemekana kutokea ambapo "kukutana kwa akili" au kwa "kuwa na nia zinazowiana". Ujerumani ina mtazamio maalum kuhusu mikataba, ambayo inayusisha sheria ya mali. Kanuni ya dhana ya kiakili (Abstraktionsprinzip wanayoitumia, inamaanisha kuwa wajibu wa kibinafsi wa mkataba unaundwa kando na jina la mwenye mali yanayokabidhiwa. Wakati ambapo mikataba inavunjwa kwa sababu fulani (kwa mfano mnunuzi wa gari amelewa kiasi kwamba hana uwezo wa kisheria wa kufanya mkataba) Wajibu wa kimkataba wa kulipa unaweza kuvunjwa tofauti na jina la mwenye gari. Sheria ya kutajirika kusio kwa haki, badala ya sheria tya mkataba, basi inatumika kurudisha jina kwa mmiliki halali.
Sheria ya ukiukaji wa wajibu
Sheria ya ukiukaji wa wajibu, ambayo wakati mwingine huitwa kosa la jinai, ni makosa ya raia. Kuwa na kosa la ukiukaji wa wajibu, mtu lazima awe amekiuka wajibu aliukwa anafaa kumtendea mty mwingine, au kukiuka haki fulani ya awali ya kisheria. mfano unaweza kuwa kumgonga mtu kimakosa na mpira wa mchezo wa kriketi. Chini ya sheria ya uzembe, ambayo ndiyo aina ya ukiukaji wa wajibu maarufu zaidi, mtu aliyepatwa na madhara anaweza kuomba fidia kwa ya majeraha yake kutoka kwa mtu mwenye uwajibikaji. Kanuni za uzembe zinaonyeshwa na kesi ya Donoghue dhidi ya Stevenson. Rafiki mmoja wa Bi. Donoghue aliagiza chupa isiyopenyeka nuru la pombe ya tangawizi (iliyokusudiwa kutumika na Bi. Donoghue) katika mkahawa katika eneo la Paisley. Baada ya kunya kunya nusu ya bia ile , Bi, Donoghue alimimina iliyosalia katika bilauri. Mabaki yaliyooza ya konokono yalielea juu ya pombe. Alidai kuwa alipigwa na bumbuwazi, na kupata ugonjwa wa kuchomeka ndani ya matumbo, na ilimbidi kumpeleka mtengenezaji pombe kwa kuruhusu kinywaji kuchafuka ovyo. Nyumba ya Mabwana iliamua kwamba mtengezaji pombe aliwajibika kwa ugonjwa wa Bi. Donoghue. Bwana Atkin alikuwa na mtazamo maalum wa kimaadili, na akasema,
Dhima ya upuuzaji ... bila shaka ina msingi wake katika mawazo ya kijumla ya umma kuhusu makosa ya kimaadili amabyo mkosaji lazima alipe ... Kanuni ya kuwa unafaa kumpenda adui yako, kisheria inakuwa, haufai kumjeruhi jirani yako; na swali la wakili, nani ndiye jirani yangu? linapokea jibu lenye vikwazo. Lazima uwe na uwangalifu wa kuepuka na vitendo au visa ambapo hautendi lolote inapofaa, ambavyo unaweza kutazamia kuwa vikamjeruhi jirani yako.
Huu ulikuwa msingi wa kanuni nne za upuuzaji; (1) Bwana Stevenson alimdai Bi. Donoghue wajibu wa kujali wa kuuza vinywaji salama (2) yeye alivunja wajibu wake wa kujali (3) madhara hayangefanyika isipokuwa kwa kuvunja kwake kwa wajibu wa kujali na (4) tendo lake lilikuwa sababau ya karibu, au haikuwa tokeo la mbali, la madhara yaliyompata mtu fulani. Mfano mwingine wa ukikaji wa wajibu unaweza kuwa wa jirani ambaye anapiga kelele nyingi sana na na mashine katika nyumbani kwake. Chini ya dai la kero kelele hiyo inaweza kukomeshwa. Ukiukaji wa wajibu pia inaweza kuhusisha vitendo vya kimakusudi, kama vile ushambulizi, vita au kuvuka na kuingia katka maeneo yaliyopigwa marufuku. Sheria ya ukiukaji wa wajibu inayofahamika vyema ni ile ya kumharibia mtu jina, ambayo inafanyika, kwa mfano, wakati gazeti linapochapisha madai yasiyokuwa na msingi ambayo yanaharibu sifa ya mwanasiasa fulani. Ukiukaji wa wajibu ambao ni mbaya zaidi ni zile wa kiuchumi, ambao huwa msingi wa sheria ya ajira katika baadhi ya nchi kwa kufanya vyama vya kibiashara kuwa na dhima kwa sababu ya migomo, Wakati ambapo amri ya kisheria haipatiani kinga.
Sheria ya mali
Sheria ya mali inatawala vitu vya thamani ambavyo watu huvitambua kama 'vyao'. Mali ya kweli wakati mwingine huitwa 'mali isiyohamishika' inahusu umiliki wa ardhi na vitu vilivyojikita katika ardhi hiyo. Mali ya kibinafsi, inaashiria mambo mengineyo; vyombo vinavyowezwa kusongeshwa, kama vile tarakilishi, magari, mapambo na mikate au turathi haki, kama vile akiba na hisa. Haki ya in rem ni haki ya kipande maalum cha mali, ikitofautishwa na haki in personam ambayo inaruhusu fidia kwa hasara, lakini si kwa kurudishiwa kitu fulani. Sheria ya ardhi inajumuisha msingi wa aina nyingi za sheria za mali, na ndiyo ngumu zaidi. Inahusisha mogeji, mikataba ya kukodisha, leseni, maagano, ruhusa na mifumo ya kisheria kwa usajili wa ardhi. Kanuni kuhusu matumizi ya ardhi ya kibinafsi chini ya haki miliki, sheria ya kampuni, hifadhi na sheria ya biashara. Mfano wa kesi msingi ya ya sheria nyingii za mali ni Armory v Delamirie. Kijana wa kufagia chimni alipata pambo lenye mawe ya thamani. Alichukua pambo lile kwa muundaji wa vifaa vya dhahabu ili thamani yake ikadiriwe. Mwanafunzi wa muundaji wa vifaa vya dhahabu aliangalia pambo lile, akaiba mawe yale ya thamani, ma kumuambia kijana yule kuwa thamani yake ilkuwa nusu peni tatu na kuwa angeinunua. Kijana yule alimwambia kuwa angepenga arudishiwe pambo lile, kwa hivyo mwanafunzi wa muundaji vifaa alimrudishia pambo, lakini bila mawe yale ya thamani. Kijana yule alimpeleka mtengenezaji wa vifaa vya dhahabu kotini kwa jaribio la mwanafunzi wake kumdanganya. Bwana Hakimu Mkuu Pratt aliamua kuwa ingawa kijana hangesemekana kuwa mumiliki wa pambo lile, angefaa kutazamwa kama mpataji aliyefaa ("mpataji muwekaji") hadi mumiliki wa kiasili anapopatikana. Kwa kweli mwanafunzi na kijana yule wote walikuwa na haki ya umiliki wa pambo lile (dhana ya kiufundi, inayomaanisha kuwa kitu fulani kingeweza kumilikiwa na mtu fulani), lakini nia ya kijana yule ya kumiliki ilitazamiwa kuwa bora zaidi, kwa sababu ingeweza kudhihirishwa kuwa ya kwanza katika wakati. Umiliki unaweza kuwa sehemu tisa kwa kumi ya sheria, lakini si yote.
Kesi hii hutumika kudhihirisha mtazamo wa mali katika maeneo ya kisheria ya kawaida, kuwa mtu anayeweza kuonyesha dai bora zaidi la kipande cha mali, dhidi ya chama kingine, ndiye mumiliki. Kwa kulinganisha, mbinu ya kiklasiki ya sheria ya raia kuhusu mali, iliendelezwa na Friedrich Carl von Savigny, ni kuwa ni haki nzuri dhidi ya Ulimwengu. Wajibu, kama mkataba na ukiukaji wa wajibu hutazamwa kama haki nzuri dhidi ya watu binafsi. Dhana ya mali inaibua maswala mengi zaidi ya kifalsafa na kisiasa. Locke alidokeza kwamba "maisha, uhuru na nyumba" zetu ni mali yetu kwa sababu tunamiliki mali yetu na tunachangayana ajira yetu na mazingira yetu.
Usawa na amana
Usawa na amana ni mwili wa sheria ulioibuka nchini Uingereza kando na "shera ya kawaida". Sheria ya kawaida ilisimamiwa na mahakimu. Bwana Chansela kwa upnade mwingine, kama muwekaji dhamiri wa mfalme, angeweza kupuuza sheria iliyotengenezwa na hakimu ikiwa alifikiria kuwa ilikuwa sawa kufanya hivyo. Hili lilimaanisha kuwa usawa ulianza kufanya kazi zaidi kupitia kanuni bali si sheria ambazo hazikubadilika. Kwa mfano, ambapo mifumo ya sheria ya kawaida au sheria ya raia haiwaruhusu watu kugawa umiliki wa kutoka kwa udhibiti wa kipande kimoja cha mali, usawa unaruhusu hili kupitia mpango unaoitwa 'amana'. Kudhibitiwa kwa mali na 'wenye amana' ambapo kwa upande mwingine umiliki 'wenye manufaa' (au 'yenye usawa') wa mali ya amana inashikiliwa na watu wanojulikana kama 'wadhamini'. Wadhamini wana wajibu kwa walengwa wao wa kuyachuna vyema mali waliyokabidhiwa. Katika kesi ya awali ya Keech dhidi ya Sandford mtoto alirithi haki ya kokodisha katika soko katika eneo la Ramford, mjini London. Bw, Sandford alikabidhiwa mali hayo hadi wakati ambapo mtoto angekomaa. Lakini kabla ya hapo, kipindi cha kukodisha kilikwisha. Kabaila alikuwa (inaonekana) amemwambia Bw. Sandford kuwa hakutaka mtoto yule awe na kukodisha kupya. Lakini bado kabaila alikuwa amefurahi (inaonekana) kumpa Bw. Sandford fursa ya kukodisha. Bw Sandford aliichukua. Wakati ambapo mtoto (sasa Bw. Keech) alikuwa mkubwa, alimpeleka Bw. Sandford mahakamani kwa faida aliyokuwa akipata kwa kupata kukodisha kwa soko. Bw. Sandford alifaa kuaminika, lakini alijiweka katika nafasi ya mgongano wa maslahi. Bwana Kansela, Bwana Mfalme, alikubali na kumuamuru Bw. Sandford kutoa faida ile na kumlipa Bw. Keech. Aliandika,
Bila shaka, Bwana Mfalme LC alikuwa na wasiwasi kwamba wadhamini huenda wakatumia fursa ya kutumia mali ya amana wenyewe badala ya kuyachunga. Wadadisi wa kibiashara wanaotumia hifadhi walikuwa wamesababisha kuaguka kwa soko la hisa katika siku hizo. Wajibu mkali kwa wadhamini ulijumuishwa katika sheria ya serikali na kutumika kwa wakurugenzi wa makampuni na maafisa watendaji wakuu. Mfano mwingine wa jukumu la mdhamini unaweza kuwa kuwekeza mali vizuri au kuiuza. Hii hasa ndiyo kesi kwa fedha za pensheni , aina muhimu kwa zote ya amana, ambapo wawekezaji ndio wadhamini wa akiba za watu hadi wastaafu. Lakini amana pia zinaweza kuundwa kwa madhumuni ya hisani, mifano maarufu ikiwa Makavazi ya Uingereza au Shirika la Rockefeller.
Utaalamu zaidi
Sheria huenea mbali kuliko masomo ya msingi hadi karibu kila eneo la maisha. Ngazi tatu zimetajwa hapa ili kurahisiha majadiliano, ingawa masomo mbalimbali hufanana na kutegemeana.
Sheria na jamii
Sheria ya ajira ni somo la uhusiano wa mara tatu wa kiwandani kati ya mfanyikazi, muajiri na chama cha wafanyikazi. Hili linahusisha kupunguza kufanya biashara kwa pamoja, na haki ya kugoma. Sheria ya kuajiriwa kwa binafsi inaashiria haki za maeneo ya kazi, kama zile usalama wa kazi, afya na usalama au mshahara wa chini zaidi.
Haki za kibinadamu, haki za kiraia na sheria ya haki za kibinadamu ni maeneo muhimu katika kumhakikishia kila mtu uhuru na haki za kimsingi, Haya yanapatikana katika maadiko kama vile Azimio la Ulimwenguni la Haki za Kibinadamu, Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu (iliyoanzisha Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu) na Mswada wa Marekani wa Haki za Kibinadamu. Mkataba wa Lisbon unafanya Mkataba wa Haki za Msingi za Umoja wa Ulaya uwe na nguvu za kisheria katika nchi zote wanachama isipokuwa Polandi na Uingereza.
Utaratibu wa Kiraia na utaratibu wa jinai unahusisha kanuni ambazo mahakama lazima yafuate kadiri trial na rufaa zinapoendelea. Yote yanahusu haki ya raia kupata kuhukumiwa kwa haki au kesi yake kusikizwa kwa haki.
Ushahidi. Sheria ya ushahidi inahusu vifaa vinavyofaa kutumika mahakamani ili kesi ijengwe.
Sheria ya Uhamiaji na sheria ya utaifa zinahusu haki za wageni kuishi na kufanya kazi katika taifa ambalo si lao na kupata na kupoteza uraia. Yote yanahusu haki ya hifadhi na shida ya watu wasiokuwa na nchi
Usalama wa Kijamii. Sheria ya usalama wa kijamii inahusu haki za watu kuwa na bima ya kijamii, kama vile pesa zinazopewa watafuta kazi au faida za makazi.
Sheria ya familia inahusu kesi za ndoa na talaka proceedings, haki za watoto na haki za kuwa na mali na pesa ikiwa wenye kufanya ndoa watatengana.
Sheria na biashara
Sheria ya kikampuni ilitokana na sheria ya amana, ikitegemea kanuni ya kutenganisha umiliki na udhibiti. Sheria ya kisasa ya kampuni ilianza na Sheria ya Kampuni za Pamoja za Akiba ya mwaka 1856, iliyopitishwa nchini Uingereza, ambayo iliwapa wawekezaji mbinu rahisi ya usajili ili kupata dhima ya kupimika chini ya dhana ya mtu tofauti wa kampuni.
Sheria ya kibiashara inahusu mkataba tata wa mkataba na mali. Sheria ya shirika, sheria ya bima, bili za kubadilishana, ufilisi na Sheria ya kuufungwa kwa biashara na sheria ya uuzaji zote ni muhimu, na zinarudi nyuma hadi dhana ya Lex Mercatoria ya zama za kati. Sheria ya Kuuza Bidhaa ya Uingereza na Kodi Sawa ya Biashara ya Marekani ni mifano ya kanuni za kibiashara ya sheria ya kawaida
Sheria ya maji na Sjeria ya Maji zinaweka muundo msingi wa biashara huru na biashara Duniani kote Baharini, ambapo yamo nje ya eneo la udhibiti wa nchi fulani. Makampuni ya meli yanafanya kazi kwa kutumia kanuni za kawaida za sheria ya biashara, ambazo zimefanywa kuwa jumla kwa soko la kimataifa. Sheria ya maji inajumuisha masuala muhimu kama vile kama vile kuokoa vifaa kutoka baharini, lieni za maji, na majeraha kwa abiria.
Miliki Sheria inalenga aims at safeguarding creators and other producers of intellectual goods and services. These are legal rights (copyrights, trademarks, patents, and related rights) which result from intellectual activity in the industrial, literary and artistic fields.
Fidia inashughulika na kupata mapato ya mtu mwingine, bali si fidia kwa hasara ya kibinafsi
Kutajirika isipofaa ndiyo nguzo ya tatu ya sheria ya raia (pamoja na mkataba na ukiukaji wa wajibu). Wakati ambapo mtu fulani ametajirishwa isipofaa (au kuna "kutokuwepo kwa msingi" wa biashara) kwa gharama ya mawingine, tukio hili linazalisha haki ya fidia ili kugeuza faida hiyo.
Sheria na vikwazo
Sheria ya kodi inahusu kanuni kuhusu kodi ya thamani iliyoongezwa, kodi ya kampuni, kodi ya mapato.
Sheria za kibenki na kanuni za kifedha zinaweka viwango vya chini zaidi kuhusu idadi ya mtaji ambao benki zinaweza kuwa nao, na sheria kuhusu utendaji bora wa uwekezaji. Hili ni kwa minajili ya kuhakikisha ulinzi dhidi ya taabu za kiuchumi, kama vileKunguka kwa soko la Wall Street mnamo mwaka wa 1929.
Vikwazo vinashughulika na utoaji wa huduma za umma na usimamizi wa vifaa vya umma.Sheria ya maji ni mfano mmoja. Hasa tangu ubinafshaji uwe maarufu na uchukue usimamizi wa huduma kutoka kwa sheria ya umma, makampuni ya kibinafsi ambayo hapo yalikuwa yakifanya kazi iliyodhitiwa na serikali hapo awali yamefungwa na vyeo mbalimbali vya wajibu wa kijamii. Nishati, gesi, mawasiliano na maji zinadhibitiwa na viwanda katika nchi nyingi za OECD.
Sheria ya mashindano, nchini Marekani inajulikana kama sheria dhidi ya amana, ni eneo linalozidi kubadilika ambalo lilianza katika kutokana na amri za Kirumi dhidi ya kuweka bei na mafundisho ya Uingereza ya biashara ya makini. Sheria ya kisasa ya mashindano inatokana na sheria za Marekani dhidi ya biashara za magendo na dhidi ya ukiritimba (Sheria ya Sherman na Sheria ya Clyaton) ya mwisho wa karne ya 20. Inatumika kudhibiti biashara zinazojaribu kutumia ushawishi wao wa kiuchumi kubadilisha biashra za sokoni bila kujali maslahi ya mnunuzi.
Sheria ya mnunuzi inaweza kujumuisha chochote kuanzia kanuni kuhusu vifungu vya mikataba ambavyo si sawa hadi maelekezo kuhusu bima ya mizigo ya ndege.
Sheria ya mazingira inazidi kuwa muhimu, hasa katika mwanga wa Itifaki ya Kyoto na hatari inayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya anga. Ulinzi wa kimazingira pia intumika kuwaadhibu wanaoharibu mazingira katika mifumo ya kisheria ya kiinchi
Mifumo ya sheria
Kwa ujumla, mifumo ya kisheria inaweza kugawanywa kati ya mifumo ya kisheria ya kiraia na mifumo ya kisheria ya kawaida. Maneno "sheria ya kiraia" yanayoashiria mfumo wa kisheria hayapaswi kuchanganyishwa na "sheria ya kiraia" kama kundi la masomo ya kisheria ambayo ni tofauti na sheria ya umma au ya jinai. Aina ya tatu ya mfumo wa kisheria—inayokubalika bado na baadhi ya nchi ambazo zina utengano wa kanisa na taifa—ni sheria sheria ya kidini, ambayo ina msingi wake katika maandiko ya kidini. Aina ya mfumo amabo nchi inatumia kutawala mara nyingi kudhamiriwa na historia yake, uhusiano wake na nchi zingine au kushikilia kwake kwa viwango vya kimataifa. Vyanzo ambavyo maneneo fulani ya kisheria hutumia kama kama zenye uwezo wa kuwa nguvu za kisheria ndizo sifa fafanuzi za mfumo wowote wa kisheria. Hata hivyo, uainishaji ni jambo la umbo kuliko maana, kwani sheria sawa mara nyingi hutawala.
Sheria ya kiraia
Sheria ya kiraia ni mfumo wa kisheria unaotumika katika nchi nyingi Duniani. Katika sheria ya kiraia vyanzo vinavyotambulika kama kuwa na mamlaka, ni, haswa, uundaji wa sheria—haswa sheria zilizoandikwa katika katiba au amri zinazopitishwa na serikali—na tamaduni. Sheria za kuandikwa zinapatikana hata katika miaka mingi ya awali , huku mfano mmoja ukiwa Codex Hammurabi ya Kibabeli. Mifumo ya sheria za kiraia ya kisasa inatokana na mazoezi ya kisheria ya Dola la Kirumi ambalo maadiko yake yalipatikana katika Ulaya ya Zama za Kati. Sheria ya Kirumu katika siku za Jamhuri ya Kiruma na Dola la Kirumi lilitegemea sana utaratibu, na ilikosa daraja la kitaaluma. Badala uake mtu wa kawaida aliyeitwa, iudex, alichagukiwa kufanya uamuzi. Kesi za awali hazikuripotiwa, kwa hivyo sheria yoyote yenye msingi katika kesi iliyoibuka ilifichwa na hata kutotambulika. Kila kesi ilikuwa ilimuliwe upya kutokana na sheria za nchi, ambayo ni sawa na kupungua kwa umuhimu (kinadharia) wa uamuzi wa mahakimu kwa kesi za siku za usoni kwa mufumo ya kisheria siku za leo. Katika kipindi cha karne ya 6 NK katika Dola la Mashariki la Roma, Kaisari Justinian I aliandika na kuzikusanya pamoja sheria ambazo zilikuwa zinapatikana hapo awali katika Roma, ambapo kile kilichobakia kilikuwa sehemu moja juu ya ishirini ya kiwango cha maandiko ya kisheria kutoka awali. Hili ikawa inafahamika kama Corpus Juris Civilis. Kwa mujibu wa mwanahistoria mmoja wa kisheria, "Justinian alitazama kwa uangalifu hadi miaka ya dhahabu ya nyuma ya sheria ya Kirumi na alilenga kuirejesha hadi upeo wake wa karne tatu za awali." Wakati uo huo, Ulaya ya Magharibi ilitumbukia polepole katika Zama za Giza, na haikuwa hadi karne ya 11ambapo wasomi katika Chuo Kikuu cha Bologna walipoyagundua upya maandiko yaliyokuwa yamepotea na kuyatumia kuzitafsiri sheria zao. Maandiko ya sheria za kiraia yenye msingi unaofanana kwa karibu na sheria ya Kirumu, sambamba na ushawishi mchache kutoka sheria za kidini kama vile sheria ya Kikanoni na sheria ya Kiislamu, iliendelea kuenea kote baranii Ulaya hadi Kutaalmika; kisha, katika karne ya 19, Ufaransa, na Sheria iliyoandikwa ya Kiraia, na Ujerumani, Bürgerliches Gesetzbuch, zilifanya sheria zao zilizokuwa zimeandikwa kuwa za kisasa. Sheria hizi mbili zilizoandikwa zilisukuma vilivyo si tu mifumo ya kisheria ya nchi katika Bara Ulaya (kama vile Ugiriki), lakini pia tamaduni za kisheria za Ujapani na Kikorea. Leo, cnhi ambazo zina mifumo ya kisheria ya kiraia ni kama vile Urusi na Uchina na maeneo mengi ya Marekani ya Kati na Marekani ya Kilatini. Marekani inafuata sheria ya kawaida inayofafanuliwa hapa chini.
Sheria ya kawaida na usawa
Sheria ya kawaida na usawa ni mifumo ya kisheria ambapo uamuzi wa mahakama yanakubalika wazi kuwa vyanzo vya sheria."Mafundisho ya utangulizi", au stare decisis (Kilatini kwa "kusimama kwa uamuzi") unamaanisha kuwa sumauzi unaofanywa na mahakama yenye mamlaka kubwa yanafunga mahakama yenye mamlaka ya chini. Mifumo ya kisheria ya kawaida hutumia amri mara chache sana, zinazopitishwa na bunge, lakini huenda zikafanya jaribio ambalo si la kitaratibu kuandika sheria zao kuliko katika "mfumo wa sheria wa kiraia". Sheria ya kawaida ina asili yake nchini Uingereza na imerithiwa na karibu nchi zote ambazo hapo awali zilihusika na Dola la Uingereza (isipokuwa Malta, Scotland, na jimbo la Marekani la Louisiana, na jimbo la Kanada la Quebec). Katika Uingereza wakati wa zama za kati, ushindi wa Norman ulisababisha kuungana kwa desturi mbalimbali za kikabila na hivyo basi kuunda sheria ya "kawaida" ya nchi yote. Labda ikisukumwa na mazoea ya kisheria ya Kiislamu wakati wa Krusedi, sheria ya kawaida iliendelea ambapo Mfalme wa Kiingereza alikuwa amefanywa kuwa dhaifu na gharama kubwa ya vita vywa kudhibiti sehemu kubwa za Ufaransa. Mfalme Yohana alikuwa amelazimishwa na mabaroni wake kutia saini hati iliyoweka vikwazo kwa mamlaka yake ya kupisha sheria. "Mkataba huu mkuu" au Magna Carta wa mwaka 1215 pia ulihitaji jopo la mahakimu wa Mfalme kufanya mikutano yao ya kimahakama na uamuzi wao katika "mahali maalum" badala ya kutoa haki ya kibepari katika maeneo yaliyokuwa magumu kutabiri kote. Kundi la mahakimu walsomi na waliokolea walipata jukumu muhimu katika kuunda sheria chini ya mfumo huu, na ikilinganishwa na wenzao Barani Ulaya mahakama ya Uingereza ilikuwa na urasimu mwingi zaidi. Kwa mfano, mnamo mwaka wa 1297, wakati ambapo mahakama kuu ya Ufaransa yalikuwa na mahakimu hamsini na wawili, Mahakama ya Uingereza ya Maombi ya Kawaida yalikuwa na watano. Mahakama haya yenye nguvu na yaliyoshikamana yalisababisha mfumo wa kikiritimba. Kufuatana na hilo, kadiri wakati ulivyopita, idadi iliyoongezeka ya raia waliomba Mfalme kupuuza sheria ya kawaida, na kwa niaba ya Mfalme Bwana Chansela alitoa uamuzi kufanya kile ambacho ni sawa kwa kila kesi. Kuanzia wakati wa Thomas More, wakili wa kwanza kuteuliwa kama Bwana Chansela, mwili wa kimfumo wa usawa uliongezeka kando ya sheria ya kawaida yenye ukiritimba, na ilianzisha Mahakama yake ya Chancery. Mwanzoni, usawa ulikosolewa kuwa ulikosa kukosa utaratibu, na kuwa ulibadilika kulingana na urefu wa mguu wa Chansela. Lakini baada ya muda iliunda kanuni, hasa chini ya Bwana Eldon. Katika karne ya 19 mifumo hiyo miwili iliunganishwa pamoja. Katika kuendeleza sheria ya kawaida na usawa, waandishi wa kitaaluma wamekuwa na jukumu muhimu. William Blackstone, kuanzia kipindi cha 1760, alikuwa mwanachuoni wa kwanza kuelezea na kufunza usawa. Lakini kwa kuelezea tu, wasomi walitafuta melezo na miunso msingi walibadilisha polepole jinisi sheria ilivyofanya kazi.
Sheria ya kidini
Sheria ya kidini inatokana na maagizo ya dini. Baadhi ya mifano ni Halakha ya Kiyahudi na Sharia ya Uislamu — ambazo zote mbili zinamaanisha "njia ya kufuata" — huku sheria za Kanisa za Ukristo nazo hutumika katika madhehebu machache, kama vile Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiorthodoksi na la Anglikana.
Mara nyingi dini inadai kutobadilika kwa sheria, kwa sababu neno la Mungu haliwezi kufanyiwa marekebisho wala kupingwa na mahakimu au serikali.
Hata hivyo mfumo fasaha wa sheria kwa jumla unahitaji upanuzi upande wa binadamu. Kwa mfano, Torati au Vitabu Vitano vya Musa katika Agano la Kale. Vitabu hivyo vina kanuni na sheria za msingi za Uyahudi, ambayo baadhi ya jamii ya Kiisraeli huchagua kutumia. Halakha ni kanuni ya sheria za Kiyahudi inayofanya muhtasari wa baadhi ya ufafanuzi wa kitabu cha Talmud. Hata hivyo, Sheria za Israeli zinaruhusu mlalamikaji kuchagua mbinu za kidini ikiwa tu anataka. Mfano mwingine ni Korani ambayo ina sheria, na inakuwa kama chanzo cha sheria zaidi kupitia ufafanuzi, Qiyas (kulinganisha), Ijma (kufikia muafaka) na yaliyokwishatokea. Hili hasa hupatikana katika mkusanyo wa sheria na falsafa ya kisheria inayojulikana kama Sharia na Fiqh.
Hadi karne ya 18, Sharia ilitekelezwa kote katika Ulimwengu wa Kiislamu katika mfumo ambao haukuwa umeandikwa kwa ufasaha, huku sheria ya Mecelle ya Dola la Ottoman katika karne ya 19 ilikuwa ya kwanza kuandika vipengele vya Sharia. Tangu miaka ya kati ya 1940, majaribio yamefanywa, katika nchi nyingi, kufanya sheria hizo zifanane zaidi na hali na dhana za kisasa.
Katika nyakati za sasa, mifumo ya kisheria katika mataifa mengi ya Kiislamu hutegemea sheria za kiraia na sheria ya kawaida na pia sheria na tamaduni za Kiislamu. Katiba za baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Misri na Afghanistan, zinatambua Uislamu kama sheria ya taifa, hivyo kuyafanya mabunge katika nchi hizo yasiwe na budi kufuata Sharia. Saudia inatambua Korani kama katiba, na inatawaliwa kwa msingi wa sheria ya Kiislamu. Iran pia imeshuhudia kurudi kwa sheria ya Kiislamu katika mfumo wake wa kisheria baada ya mwaka 1979. Katika miongo michache iliyopita, mojawapo ya tofauti kuu ya harakati ya mwamko wa Kiislamu imekuwa wito wa kuirejesha Sharia, wito ambao umeibua kiasi kikubwa cha maandishi na kuathiri siasa duniani.
Nadharia ya sheria
Historia ya Sheria
Historia ya sheria inashikamana kwa karibu na maendeleo ya ustaarabu. Sheria ya Misri ya Kale, iliyorudi nyuma mbali hadi mnamo 3000 KK, ilikuwa na mkusanyiko wa sheria ambao huenda ulikuwa umegawanjwa katika vitabu kumi na viwili. Ilizingatia dhana ya Ma'at, iliyokuwa na sifa ya mapokeo, hotuba za kushawishi, usawa wa kijamii na uaminifu.
Kufikia karne ya 22 KK, mtawala wa zamani wa Kisumeri, Ur-Nammu alikuwa ameandaa mkusanyiko wa sheria, ambao ulihusisha kauli za kimjadala ("ikiwa ... basi ...").
Kufikia mwaka wa 1760 KK, Mfalme Hammurabi aliboresha zaidi Sheria ya Babeli, kwa kuikusanya na kujandika katika jiwe kubwa. Hammurabi aliweka nakala kadhaa za jiwe lile kote katika milki ya Babeli kama stelae, ili watu wote waitazame; hii ilikuja kufahamika kama Mkusanyiko wa Sheria za Hammurabi. Nakala iliyobaki ambayo haijaharibika sana wa stelae hizi iligunduliwa katika karne ya 19 na Waingereza wasomi wa mambo ya milki ya Assyria, na tangu wakati huo imenakiliwa upya na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali, zikiwemo Kiingereza, Kijerumani na Kifaransa.
Agano la Kale lilianza mnamo 1280 KK, na linachukua umbo la amri za kimaadili kama mapendekezo ya jamii nzuri.
Mji-dola wa Ugiriki ya Kale, Atheni ya Kale kuanzia karne ya 8 KK ilikuwa jamii ya kwanza kuwa na msingi wake katika kuhusisha raia kwa upana; isipokuwa wanawake na daraja la watumwa. Hata hivyo, Atheni haikuwa na sayansi ya kisheria, na hapakuwa na neno la "sheria" isipokuwa kama dhana ya kiakili tu. Bado sheria ya Ugiriki wa Kale ilikuwa na uvumbuzi mkubwa wa kikatiba katika kuendeleza demokrasia.
Sheria ya Kirumi ilisukumwa sana na falsafa ya Kigiriki, lakini maelezo yake ya kina yaliendelezwa na wanasheria wa kitaaluma, na yalikuwa magumu sana. Katika kipindi cha karne zilizopita kati ya kupanda na kushuka kwa Dola la Roma, sheria imebadilishwa ili kukabiliana na hali za kijamii zilizokuwa zikibadilika, na ilikusanywa na kuandkiwa vilivyo wakati wa utawala wa kaisari Justinian I. Ingawa ilipungua kwa umuhimu mwanzoni mwa Karne za Kati, Sheria ya Kirumi iligunduliwa upya wakati wa karne ya 11 ambapo wasomi walianza kutafiti mkusanyiko wa sheria za Kirumi na kuyatumia mawazo yao.
Katika Uingereza ya Zama za Kati, mahakimu wa Mfalme waliunda mwili wa utangulizi, ambao baadaye ulijulikana kama sheria ya kawaida. Sheria ya biashara ya Ulaya mzima iliundwa ili kuwapa wafanyabiashara uwezo wa kufanya biashara kwa kutumia viwango sawa vya mazoezi; badala ya kutumia sheria za kimtaa zenye pande nyingi. Hiyo Lex Mercatoria, mtangulizi wa sheria ya kisasa ya biashara, ilihimiza uhuru wa mkataba na kuwekwa mbali kwa mali.
Kadiri utaifa ulipozidi katika karne za 18 na 19, ndipo Lex Mercatoria ilipozidi kujumuishwa katika sheria za kimanispaa za nchi mbalimbali chini ya mkusanyiko mpya wa sheria za kiraia. Mkusanyiko wa Sheria za Napoleoni na sheria za Kijerumani ulikuwa na ushawishi mkubwa zaidi. Ikitofautishwa na sheria ya kawaida ya Uingereza, ambayo ina idadi kubwa ya sheria za kesi, mikusanyiko ya sheria katika vitabu vidogo ni rahisi kuuza nje ili mahakimu waweze kuitumia. Hata hivyo, hivi leo kuna ishara kuwa sheria ya kiraia na sheria ya kawaida zinazidi kukaribiana. Sheria ya Umoja wa Ulaya imekusanywa katika mikataba, lakini huendelezwa kupitia utangulizi unaofanywa na Mahakama ya Ulaya ya Haki.
Sheria ya Kiislamu na falsafa ya sheria zilianza katika kipindi cha Zama za Kati. Mbinu ya kisheria ya utangulizi na kufikiria kupitia mlinganisho (Qiyas) iliyotumika katika sheria ya mapema ya Kiislamu ilifanana na na ile ya baadaye ya mfumo wa Sheria ya Kawaida ya Uingereza. Hii ilitumika hasa katika shule ya Maliki ya sheria ya Kiislamu iliyopatikana sana katika eneo la Afrika Kasakazini, Uhispania wa Kiislamu na baadaye Sicily ya Kiemereti. Kati ya karne za 8 na 11, sheria ya Maliki iliendeleza taasisi nyingi zilizokuwa sambamba na taasisi za baadaye za sheria ya kawaida.
Sheria ya kale ya Uhindi na Uchina zinawakilisha mapokeo tofauti ya sheria, na kihistoria yamekuwa na shule huru za kinadharia na mazoezi.
Arthashastra, ambayo pengine iliandikwa mnamo 100 BK (ingawa ina maandiko ya awali kidogo), na Manusmriti (100–300) yalikuwa mikataba ya uanzilishaji nchini Uhindi, na ilikuwa na maandiko yanayofikiriwa kuwa wongofu wenye mamlaka wa kisheria. Falsafa kuu ya Manu ilikuwa kuvumiliana na Mfumo wa Vyama Vingi, na ilitajwa kote katika eneo la Asia ya Kusini Mashariki.
Mapokeo haya ya Kihindu, pamoja na sheria ya Kiislamu, yalibadilishwa na na sheria ya kawaida wakati ambapo Uhindi ilifanywa kuwa sehemu ya Dola la Uingereza. Malaysia, Brunei, Singapore na Hong Kong pia ilianza kutumia sheria ya kawaida, Mapokeo ya sheria ya Asia ya Kusini yanaangazia mkusanyiko maalum wa ushawishi wa kidunia na kidIni.
Ujapani ilikuwa nchi ya kwanza kuufanya mfumo wake wa sheria uwe wa kisasa sambamba na ule wa nchi za magharibi, kwa kuagiza sehemu za mkusanyiko wa sheria za Ufaransa, lakini hasa mkusanyiko wa sheria za Kijerumani. Hili lilionyesha kwa kiwango fulani hadhi ya Ujerumani kama nguvu yenye uwezo mkubwa zaidi katika kipindi cha mwisho cha karne ya 19.
Pia, sheria ya mapokeo ya Uchina ilifungua njia kwa kubadilishwa na nchi za magharibi kuelekea miaka ya mwisho ya nasaba ya Ch'ing kupitia njia ya mkusanyiko wa sheria tatu za kibinaFsi zilizokuwa na msingi katika muundo wa Ujapani wa sheria ya Ujerumani. Leo sheria ya Taiwan inabaki na mshikamano wa karibu zaidi na mkusanyiko wa sheria kutoka kipindi hicho, kwa sababu ya mgawanyiko kati ya wanataifa wa Chiang Kai-shek, ambao walitoroka kutoka sehemu hiyo, na wakomunisti wa Mao Zedong waliopata ushindi wa kudhibiti bara mnamo mwaka wa 1949. Muundombinu wa sasa wa Jamhuri ya Watu wa Uchina ilishawishika pakubwa na Sheria ya Kisoshalisti ya Umoja wa Kisovyeti, inayopea sheria ya utawala umuhimu mwingi kuliko haki za sheria ya kibinafsi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa kasi kwa viwanda, leo Uchina inapitia machakato wa wa marekebisho, angalau katika nyanja ya haki za kiuchumi, ikiwa si haki za kijamii na kisiasa. Sheria mpya ya mkataba ya mwaka wa 1999 ilikuwa ishara ya kusonga mbali na kuwa na utawala mwingi. Isitoshe, baada ya mazungumzo yaliyodumu miaka kumi na mitano, mnamo mwaka 2001 Uchina ilijiunga na Shirika la Biashara Duniani.
Falsafa ya sheria
Falsafa ya sheria kwa kawaida inaitwa jurisprudensi. Jurisprudensi unaozidi kuongezka wenyewe ni falsafa ya kisiasa, na unauliza "sheria inafaa kuwa nini?", huku jurisprudensia ya uchambuzi inauliza "sheria ni nini?". Jibu la kiutumikaji la John Austin linajibu kuwa sheria ni "amri, zinazoandamana na matishio ya vkwazo, kutoka kwa mtawala, ambaye watu wote wamezoea kumtii". Mawakili wa sheria ya kimaumbile kwa upande mwingine, kama vile Jean-Jacques Rousseau, wanadokeza kwamba sheria inaangazia sheria isiyobadilika ya tabia ya kimaumbile. Dhana ya "sheria ya kimaumbile" iliibuka katika falsafa ya Kigiriki ya zamani kwa wakati mmoja na kwa pamoja na dhana ya haki, na iliingia mkondo wa utamaduni wa Magharibi kupitia maandiko ya Thomas Aquinas na maoni ya mwanafalsafa wa Kiislamu na mwanasheria Averroes.
Hugo Grotius, mwanzilishi wa mfumo uliotegemea dhana za kiakili pekee ya sheria ya kimaumbile, alidokeza kuwa sheria inatokana na msukumo wa kijamii—jinsi Aristotle alivyokuwa amesema—na kufikiria. Immanuel Kant aliamini kuwa amri ya kimaadili inahitaji sheria "zichaguliwe kana kwamba zinafaa kushikilia kama sheria za ilimwenguni kote za kimaumbile". Jeremy Bentham na mwanafunzi wake Austin, wakimfuata David Hume, waliamini kuwa hili liliongeza utata wa "kilicho" na kile ambacho "kinafaa kuwepo". Bentham na Austin walisisitiza kuwe na sheria ya uchanya; na kuwa sheria ya kweli ni tofauti kabisa na "maadili". Kant pia alikosolewa na Friedrich Nietzsche, ambaye alikataa kanuni ya usawa, huku akiamini kuwa sheria hutokana na nia kwa nguvu, na haiwezi fanywa kuwa ya "kimaadili" au "utovu wa nidhamu".
Mnamo mwaka wa 1934, mwanafalsafa wa Kiaustria, Hans Kelsen, alizidi na mapokeo ya uchanya katika kitabu chake Nadharia Safi ya Sheria. Kelsen aliamini kuwa ingawa sheria ni tofauti na maadili, inapewa "ukawaida"; kumaanisha kuwa tunfaa kuitii. Ingawa sheria ni taarfa chanya za "ni" (k.m. faini ya kuendesha kwa kurudi nyuma katika barabara kuu ni €500); hii sheria inatuelezea kile "tunachofaa" kutenda. Kwa hivyo kila mfumo wa sheria unaweza kudadisiwa kuwa na kanuni ya msingi (Grundnorm) ianyotupea amri ya kutii. Mpinzani mkuu wa Kelsen, Carl Schmitt, alikataa uchanya na dhana ya utawala wa sheria kwa sababu hakukubali umuhimu wa kanuni za kidhana za Uchanya badala ya mitazamo na uamuzi bayana wa kisiasa. Kwa hiyo, Schmitt alipendekeza falsafa ya sheria ya maalum (hali ya dharura), ambayo ilikanusha kuwa kanuni za kisheria zingezunguka uzoefu wote wa kisiasa.
Baadaye katika karne ya 20, H. L. A. Hart alimshambulia Austin kwa kurahisisha kwake kwa suala hilo na Kelsen kwa kutunga kwake kwa mambo ya kihadithi katika kitabu cha Dhana ya Sheria. Hart alidokeza kuwa sheria ni mfumo wa kanuni, zilizogawanywa kuwa (kanuni za maadili) ambazo ndizo za kimsingi na sheria za upili (zinazowalenga maafisa kusimamia kanuni msingi). Kanuni za upili zimegawanywa zaidi kuwa sheria za uamuzi (kutatua migogoro ya kisheria), kanuni za mabadiliko (zinazoruhusu sheria kuwa tofauti) na sheria ya utambuzi(inayoruhusu sheria kutambulika kama halali). Wawili kati ya wanafunzi wa Hart waliendeleza mjadala: Ktaika kitabu chake Dola la Sheria, Ronald Dworkin alimshabulia Hart na wachanya kwa kukataa kwao la kufanya sheria iwe suala la kimaadili. Dworkin anadokeza kuwa sheria ni dhana ya "kitafsiri", inayowataka mahakimu kupata suluhisho bora zaidi kwa mgogoro wa kisheria, kwa mujibu wa mila zao. Joseph Raz, kwa upande mwingine, anawataka alitetea mtazamo wa kichanya na kukosoa mtazamo wa Hart wa "nadharia laini ya kijamii" katika kitabu chake Mamlaka ya Sheria. Raz anadokeza kuwa sheria ni mamlaka, yanayotambulika kupitia vyanzo vya kijamii na bila kurejelea hoja za kimaadili. Katika maoni yake, uainishaji wowote wa kanuni zozote zaidi ya majukumu yao kama vifaa vya kimamlaka katika upatanisha ni bora yaachiwe elimu ya jamii, badala ya falsafa ya sheria.
Uchambuzi wa kiuchumi wa sheria
Katika karne ya 18 Adam Smith aliwasilisha msingi wa kifalsafa wa kuelezea uhusiano kati ya sheria na uchumi. Taaluma hiyo ilitokana na mchango wa ukosoaji dhidi ya vyama vya wafanyikazi na sheria dhidi ya amana nchini Marekani. Watetezi wa taaluma hii waliokuwa na ushawishi mkubwa zaidi, kama vile Richard Posner na Oliver Williamson na kinachojulikana kama Shule ya Chicago ya wanauchumi na mawakili ikiwemo Milton Friedman na Gary Becker, kwa jumla ni watetezi wa uouguzaji wa udhibiti na ubinafsishaji, na ni maadui wa udhibiti wa serikali au kile wanachokiona kuwa vikwazo dhidi ya unedeshaji wa masoko huru.
Mchambuzi maarufu zaidi wa kiuchumi wa sheria ni mshindi wa Tuzo la Nobel la mnamo 1991 Ronald Coase, ambaye makala yake makuu ya kwanza, Hali ya Kampuni (1937), kulidokeza sababu za kuwepo kwa makampuni mbalimbali (makampuni, ubia, n.k.) ndiyo kuwepo kwa gharama za biashara. Binadamu ambao hufikiria kawaida hufanya biashara kupitia mikataba ya bilaterala katika masoko wazi hadi wakati ambapo gharama ya biashara kunamaanisha kuwa kutumia makampuni ya kihalmasahhuri ili kuzalisha bidha ni ya ufanisi mwingi zaidi.Makala yake makuu ya pili, Shida ya Gharama ya Kijamii (1960), yalidokeza kuwa tunaishi katika Dunia bila gharama za kibiashara, watu ambao huongea kuhusu gharama pamoja wanatengeneza mgao sawa wa rasilimali, buila kujali jinsi mahakama yanavyoweza kuamua katika migogoro kuhusu mali. Coase alitumia mfano wa kesi ya kero iliyoitwa Sturges dhidi ya Bridgman, ambapo mtengenezaji peremende ambaye alipiga kelele nyingi na daktari mtulivu walikuwa majirani na walienda mahakamani ili wajue nani kati yao ndiye angefa kuhama. Coase alisema kuwa bila kujali ikiwa hakimu aliamua kuwa mtengenezaji peremende angefaa kuwacha kutumia mashine zake, au ikiwa ingembidi daktari kuvumilia kelele ile, wote wawili wangefikia mapatano ya pamoja kuhusu nani ndiye angefaa kuhama ambayo yanafikia matokeo sawa na mgawanyo wa rasilimali. Ni kuwepo tu kwa bei za biashara kunaoweza kuzuia hili. Kwa hivyo sheria infaa kutazamia kile ambacho huenda kikafanyika, na kuongozwa na ufumbuzi wenye ufanisi. Wenye kuunda mipango serikalini wanaamini wazo kwamba sheria na vikwazo si muhimu au zenye ufanisi katika kuwasaidia watu. Coase na wengine kama yeye walitaka mabadiliko ya mbinu, ili kuweka mzigo wa ushahidi katika serikali iliyokuwa ikiingilia soko, kwa kuchambua gharama za hatua.
Elimujamii ya sheria
Somo la kijamii la sheria ni taaluma pana ya masomo inayotazama mwingiliano kati ya sheria na jamii na inahusiana kwa karibu na falsafa ya sheria, uchambuzi wa kiuchumi wa sheria na masomo maalum zaidi kama somo la jinai. Taasisi za ujenzi wa jamii na mifumo ya kisheria ni maeneo muhimu ya uchunguzi wa taaluma hii. Mwanzoni, wananadharia wa kisheria walishuku taaluma hii. Kelesen alimshambuliwa mmoja wa waanzilishi wake, Eugen Ehrlich, ambaye alitaka kuweka wazi tofauti kati ya sheria ya uchanya, ambayo mawakili wanajifunza na kutumia, na aina zingine za 'sheria' au kanuni za kijamii zinazodhibiti maisha ya kila siku, na kwa jumla kuzuiwa migogoro isiwafikie mawakili mahakamani.
Katika kipindi cha mwaka 1900 Max Weber alifafanua mbinu yake ya "kisayansi" ya sheria, huku akitambua "umbo la kimantiki ya sheria" kama aina ya utawala, ambao si chanzo cha watu lakini kwa dhana za kiakili. Umantiki wa kisheria yalikuwa maneno yake aliyoyatumia kuelezea mwili wa sheria zinazoeleweka na zinazoweza kuhesabika na zilikuwa hatua ya kwanza ya maendeleo ya kisasa ya kisiasa na taifa la ukiritimba la kisasa na kuibuka sambamba na ubepari. Msomi mwingine wa somo la jamii, Émile Durkheim, aliandika katika Mgawanyo wa Ujira na Jamii kuwa kadiri jamii inavyozidi kuwa kubwa, ndivyo mwili wa sheria ya kiraia unaohusika hasa na fidia unapozidi kukuwa kwa gharama ya sheria za jinai na vikwazo vya kisheria.
Ili kupitisha sheria, idadi kubwa ya Wabunge lazima wapige kura ili muswada (sheria inayopendekezwa) upitishwe katika kila nyumba. Kawaida kutakuwa na kusoma kwingi na marekebesho mengi yaliyopendekezwa na makundi tofaiti ya kisiasa. Ikiwa nchi ina katiba inayofuatiliwa vyema, idadi maalum ya mabadiliko katika katiba yanahitajika, hivyo kufanya iwe gumu kubadilisha sheria. Serikali kwa kawaida huongoza mchakato huo, ambao unaweza kujumuisha Wabunge (k.m. nchini Uingereza na Ujerumani). Lakini katika mfumo wa kiraisi, serikali inachagua baraza la mawaziri kutawala kutoka kwa washirika wake kisiasa ikiwa wamechaguliwa au la (k.m. nchini Marekani au Brazili), na jukumu la bunge linapunguza liwe kukubali au kukataa.
Serikali
Mtendaji katika mfumo wa kisheria hutumika kama kituo cha serikali cha mamlaka ya kisiasa. Katika mfumo wa kibunge, kama vile nchini Uingereza, Italia, Ujerumani na Ujapani, mtendaji hujulikana kama serikali, na huwa na wanachama wa bunge. Mtendaji huchaguliwa na Waziri Mkuu au Chansela, ambaye ofisi yake ina nguvu za chini ya imani ya bunge. Kwa sababu uchaguzi wenye watu wengi huteua vyama vya kisiasa kutawala, kiongozi a chama anaweza kubadilika katika kipindi kabla ya uchaguzi mwingine. Mkuu wa Taifa ni kando na mtendaji, na kimfano hupitisha sheria na huwa kama mwakilishi wa nchi. Baadhi ya mifano ni Rais wa Ujerumani (anayeapishwa na Bunge); Malkia wa Uingereza (wadhifa wa kurithi), na Rais wa Austria (anachaguliwa kwa kura ya wengi). Mfano mwingine muhimu ni mfumo wa kirais, unaopatikana nchini Ufaransa, Marekani na Urusi. Katika mifumo ya kirais, mtrndaji huwa kama mkuu wa taifa na mkuu wa serikali, na ana nguvu za kuchagua baraza la mawaziri pekee yake. Chini ya mfumo wa kirais, tawi la mtendaji ni kando na bunge ambapo haiwajibiki mbele ya bunge.
Ingawa jukumu la mtendaji ni tofauti toka nchi moja hado nyingine, kawaida itapendekeza wingi wa sheria, na kupendekeza ajenda ya serikali. Katika mifumo ya kirais, mtendaji mara nyingi ana nguvu za kukataa sheria. Mara nyingi mtendaji katika mifumo yote ana wajibu wa sera za mahusiano ya nje, jeshi na polisi na urasimu. Mawaziri au maafisa wengine wanasimamia ofisi za nchi, kama vile wizara ya nje au wizara ya ndani. Uchaguzi wa mtendaji tofauti kwa hivyo ina uwezo wa kupindua mtazamo wa nchi nzima wa serikali.
Jeshi na polisi
Ingawa mashirika ya kijeshi yamekuwepo kwa muda mrefu kama serikali yenyewe, dhana la kikosi cha polisi kilicho tayari ni dhana ya kisasa. Mfumo wa Uingereza ya Zama za Kati ya mahakama ya jinai ya kusafiri, au assize, ilitumia kesi za maonyesho na unyongaji hadharani kufanya jamii ziwe na hofu na hivyo kudumisha udhibiti. Polisi wa kwanza wa kisasa pengine walikuwa wale wa Paris wa karne ya 17, katika mahakama ya Louis XIV, ingawa Polisi wa Mkoa wa Paris ndio wanadai kuwa wao ndio waliokuwa wa kwanza kuvaa sare.
Weber yu maarufu kwa kudokeza kwamba taifa ni lile ambalo linadhibiti kihalali utumizi wa kipekee wa vurugu. Majeshi na askari wanalinda usalama kufuatana na amri ya serikali au mahakama. Maneno taifa lililopangarayika yanaashiria taifa ambalo haliwezi kutekeleza au kulazimisha sera; askari wao na majeshi hawana uwezo wa kulinda usalama na amani na jamii inaelekea vurugu pekee, wakati serikali inapokosekana.
Urasimu
Asili ya neno "Urasimu" kwa Kiingereza (bureaucracy) ni neno la Kifaransa la "ofisi" (bureau) na neno la Kigiriki cha Zamani cha "nguvu" (kratos). Kama tu wanajeshi na polisi, watumishi wa mfumo wa kisheria wa serikali na miili inayounda urasimu wake hufuata maagizo ya Mtendaji. Mojawapo ya marejeo kwa dhana yalifanywa Baron de Grimm, mwandishi wa Kijerumani aliyeishi nchini Ufaransa. Mnamo mwaka wa 1765 aliandika,
Roho halisi ya sheria nchini Ufaransa ni urasimu amabo marehemu Monsieur de Gournay alikuwa akilalamika sana kuhusu; hapa ofisi, makarani, makatibu, wasimamizi na wanaonuia kufanya kazi fulani hawaapishwi kufaidi maslahi ya umma, kwa hakika maslahi ya ummayanaonekana kuanzishwa ili ofisi hizo ziwepo.
Wasiwasi kuhusu "utawala wa kiofisi" bado ni kawaida, na utendaji wa watumishi wa umma kawaida hutofautishwa na wa kampuni za kibinafsi zinazoendeshwa na lengo la faida. Kwa kweli kampuni za kibinafsi, hasa zile kubwa, pia zina urasimu. Mtazamo mbaya wa "urasimu" kando, huduma za umma kama vile elimu, afya na shughuli za polisi au uchukuzi wa umma ni kazi muhimu nchi hivyo basi kufanya urasimu wa umma chanzo cha nguvu za serikali. Akiandika mapema katika karne ya 20, Max Weber aliamini kuwa sifa muhimu ya nchi iliyoendelea ilikuwa imekuwa msaada wake wa kirasimu. Weber aliandika kuwa sifa za kawaida za urasimu wa kisasa ni kuwa maafisa wanafafanua lengo lake, wigo wa kazi umefungwa na kanuni, usimamizi unajumuisha wataalamu wa wataalamu wa kitaaluma, amabo ambao husimamia kuanzia juu kuenda chini, wakiwasiliana kupitia kuandika na kufunga uwezo wa wafanyikazi wa umma kufanya watakavyo kwa kutumia kanuni.
Taaluma ya sheria
Hitimisho la utawala wa sheria ni kuwepo kwa taaluma ya kisheria yenye uhuru wa kutosha wa kuweza kuomba mamlaka ya mahakama huru; haki ya usaidizi kusaidiwa na wakili mahakamani uanatokana na hitimisho hili—nchini Uingereza kazi ya wakili inatofautishwa na ile ya mshauri wa kisheria. Kama mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu yanavyosema, sheria inafaa kupatikana na kila mtu na waty wanfaa kutabiri jinsi sheria itakavyowaathiri. Ili kudumisha utaaluma, zoezi la sheria kawaida linachungwa na serikali au mwili huru kama vile chama cha mawikili, baraza la mawakili au jamii ya sheria. Mawakili wa kisasa wanapata utambulisho maalum wa kisheria kupitia taratibu maalum za kisheria (k.m. mafanikio katika mitihani), yanahitajika na sheria ili kuwa na cheti maalum (elimi ya kisheria inayompa mwanafunzi Shahada ya Sheria, Shahada ya Sgeria ya Kiraia, au Shahada ya Juris Doctor), na zinawekwa ofisini kwa kutumia fomu za kisheria za kuapishwa (kukubaliwa katika baraza la mawakili). Nchi nyingi za Kiisalmu zina sheria sawa kuhusu elimu ya kisheria na taaluma ya kisheria, lakini zingine bado zinaruhusu mawakili wenye mafunzo katika sheria ya Kiislamu ya jadi katika taaaluma ua sheria katika mahakama ya hadhi ya kibinasfi. Nchini Uchina na katika nchi zingine za ulimwengu unaoendelea hakuna watu wa kutosha wenye mafunzo ya kisheria kufanya kazi katika mifumo ya mahakama iliyopo katika nchi hizo, na, kufuatana na hilo, viwango rasmi si vikali sana.
Baada ya kupata kukubalika, wakili mara nyingi atafanya kazi katika kampuni ya sheria, katika vyumba kama wakili wa kipekee, katika wadhifa wa kiserikali au katika shirika la kibinafsi kama mshauri wa ndani. Isitoshe wakili anaweza kuwa utafiti wa kisheria|mtafiti wa kisheria anayepeana uatafiti wa kisheria unapoitishwa kupitia maktaba, huduma ya kibiashara au kazi isiyokuwa na muajiri mmoja. Watu wengi wenye mafunzo katika sheria walitumia utafiti wao katika taaluma nyingine tofauti kabisa. Adhimu kwa zoezi la sheria katika mapokeo ya sheria ya kawaida ni utafiti wa kisheria kujua hali ya wakati wa sasa wa sheria. Hili linahushisha kuchunguza ripoti za kesi, majarida ya kisheria na sheria. Zoezi la sheria pia inahusu kuandika hati kama vile kuiitia kwa mahakama, [[brifu [sheria)|brifu]], mikataba, au amana. Majadiliano na ujuzu wa kusuluhisha migogoro (ikijumuisha mbinu za ADR) pia ni muhimi kwa zoezi la sheria, ikitegemea na aina ya taaluma.
Mashirika ya kijamii
Dhana ya Kiripablikani wakati kulipokuwa na madaraja mbalimbali ya kijamii ya "mashirika ya kijamii" ilianzia wakati wa Hobbes na Locke. Locke aliona mashirika ya kijamii kama watu wenye "sheria sawa na mahakama kurejelea , yenye mamlaka ya kuamua utata baina yao." Mwanafalsafa wa Kijerumani Georg Wilhelm Friedrich Hegel alitofautisha "taifa" na "mashirika ya kijamii" (burgerliche Gesellschaft) katika kitabu chake Vipengele vya Falsafa ya Sawa. Hegel aliamini kuwa mashirika ya kijamii na taifa zilikuwa kinyume kabisa, katika mpangilio wa nadharia yake ya historia. Taifa la kisasa lenye pande hizi mbili–mashirika ya kijamii lilizaliwa tena katika nadharia za Alexis de Tocqueville na Karl Marx. Siku hizi katika nadharia ya wakati wa baada ya kisasa za mashirika la kijamii lazima iwe chanzo cha sheria, kwa kuwa msingi ambapo watu wanaunda maoni na kushwishi yale wanayoamini sheria inafaa kuwa. Kama wakili wa Kiaustralia na mwandishi Geoffrey Robertson QC alivyoandika kuhusu sheria ya kimataifa,
... mojawapo ya vyanzo vyake vya kisasa inapatikana katika majibu ya kawaida ya wanaume na wanawake, na mashirika yasiyo ya kiserikali, amabyo wengi huunga, kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu amabyo wengi huona kwenye runinga wakiwa sebuleni nyumbani mwao.
Uhuru wa kujieleza, uhuru wa kujumuika na sheria zingine nyingi za kibinafsi zinawaruhusu watu kukusanyika, kujadili, kukosoa na kufanya serikali zao kuwajibika, ambapo msingi wa demokrasia ya majadiliano inaibuka. Watu wanapozidi kujihusisha mamlaka ya kisheria na na kuwa na uwezo wa kubadilisha jinsi mamlaka ya kisiasa yanapotumika maishani mwao; ndivyo sheria inapozidi kuwa halali kwa watu. Taasisi ambazo ni za kawaida sana za mashirika ya kijamii ni masoko ya kibiashra, kampuni zenye malengo ya kupata faida, familia, vyama vya kibiashara, hospitali, vyuo vikuu, shule, mashirika ya msaada, vilabu vya kujadili, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vitongoji, makanisa, na vyama vya kidini.
Tazama pia
Haki za kibinadamu
Uchumi
Historia
Sayansi ya Kisiasa
Falsafa
Tanbihi
https://www.path-2-happiness.com/sw
Marejeo
Printed sources
. See original text in Perseus program.
{{cite journal |last=Coase |first=Ronald H. |authorlink=Ronald H. Coase |year=1960 |month=Oktoba |title=The Problem of Social Cost (this online version excludes some parts) |journal=Journal of Law and Economics |volume=3 |pages=1–44 |url=http://www.sfu.ca/~allen/CoaseJLE1960.pdf The Problem of Social Cost |accessdate=2007-02-10 |doi=10.1086/466560 |archive-date=2005-03-31 |archive-url=https://web.archive.org/web/20050331232727/http://www.sfu.ca/~allen/CoaseJLE1960.pdf |dead-url=yes }}
Hamilton, Michael S., and George W. Spiro (2008). The Dynamics of Law, 4th ed. Armonk, NY: M.E. Sharpe, Inc. ISBN 978-0-7656-2086-6.
Locke, John (1689). Second Treatise''
Online sources
Viungo vya nje
Legal news and information network for attorneys and other legal professionals
Encyclopaedic project of academic initiative in Jurispedia
Legal articles, news, and interactive maps
WorldLII - World Legal Information Institute
CommonLII - Commonwealth Legal Information Institute
AsianLII - Asian Legal Information Institute (AsianLII)
AustLII - Australasian Legal Information Institute
BaiLII - British and Irish Legal Information Institute
CanLII - Canadian Legal Information Institute
NZLII - New Zealand Legal Information Institute
PacLII - Pacific Islands Legal Information Institute
Elimu jamii
Historia
Falsafa |
73 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Siasa | Siasa | Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali za jamii, kama vile mji, taifa, au hata dunia nzima (siasa ya kimataifa).
Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.
Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.
Hapa chini, mifumo mbalimbali ya kisiasa huelezwa kifupi:
Utawala wa Kifalme
ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya dola na ya serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme.
Utawala wa Kiimla
ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru katika maamuzi.
Utawala finyu
ni mfumo unaowapa wachache kati ya wengi nguvu za maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila.
Utawala wa Umma
ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza, hivyo unatoa fursa ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama demokrasia na umegawanyika katika sehemu zifuatazo:
Demokrasia Chama
ni aina ya demokrasia ya kura. Inashirikisha watu wote kuwa wanachama.
Demokrasia Baguzi
ni aina ya demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi.
Demokrasia Duni
ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mfano: chama - serikali.
Demokrasia Endelevu
ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya usawa na kupinga matabaka katika jamii.
Demokrasia Shirikishi
katika aina hii ya demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi.
Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge huwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi.
Siasa |
78 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ushairi | Ushairi | Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha. Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi. Kinyume chake ni nathari.
Inawezekana kutunga mashairi yenyewe au kutumia lugha ya kishairi katika aina nyingine za sanaa, kwa mfano tamthiliya au nyimbo.
Ushairi una historia ndefu. Kwa mfano, mwanafalsafa Aristotle katika kitabu chake Ushairi ("Poetics" kwa Kiingereza) anachunguza matumizi yake katika hotuba, tamthiliya, nyimbo na futuhi.
Ushairi una vipera vitano ambavyo ni:
1. nyimbo
2. ngonjera
3. mashairi mepesi
4. maghani
5. tendi
6. rara
7. rara nafsi
Maana na tafsiri ya ushairi kulingana na washairi wakubwa
Katika kujenga hoja mbalimbali za ushairi ni nini. Wakongwe na magwiji wa ushairi wa awali walieleza maana mbalimbali za ushairi kulingana na utunzi. Wakongwe hao waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi.
Marejeo
Fasihi |
654 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Lugha%20saidizi%20ya%20kimataifa | Lugha saidizi ya kimataifa | Lugha saidizi ya kimataifa ni lugha ya kuundwa iliyoundwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya watu toka mataifa mbalimbali. Lugha saidizi ya kimataifa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto. Nyingine ni kama Kivolapuki, Kiido, Kiinterlingua na Kislovianski.
Lugha saidizi ya kimataifa
nl:Kunsttaal#Internationale hulptalen |
660 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hisabati | Hisabati | Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu.
Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo.
Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra.
Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات (halisi: hesabu (wingi)).
Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake.
{|style="border:1px solid #ddd; text-align:center; margin:auto" cellspacing="15"
||| || ||
|-
|Mantiki ya kihisabati || Nadharia ya seti || Nadharia ya kategoria || Nadharia ya kuhesabu
|}
Historia ya Hisabati
Mwanahisabati Mjerumani Carl Friedrich Gauss aliita hisabati malkia wa sayansi ambayo inasaidia katika uvumbuzi wa kisayansi. Somo la hisabati lilikita mizizi kwa sababu ya uchu wa wanasayansi kupenda kutatua shida kama vile za biashara, ugavi wa ardhi na masomo ya sayari na katika kukisia uzani.
Tanbihi
Marejeo
Courant, Richard and H. Robbins, What Is Mathematics? : An Elementary Approach to Ideas and Methods, Oxford University Press, USA; 2 edition (July 18, 1996). ISBN 0-19-510519-2.
du Sautoy, Marcus, A Brief History of Mathematics, BBC Radio 4 (2010).
Eves, Howard, An Introduction to the History of Mathematics, Sixth Edition, Saunders, 1990, ISBN 0-03-029558-0.
Kline, Morris, Mathematical Thought from Ancient to Modern Times, Oxford University Press, USA; Paperback edition (March 1, 1990). ISBN 0-19-506135-7.
Oxford English Dictionary, second edition, ed. John Simpson and Edmund Weiner, Clarendon Press, 1989, ISBN 0-19-861186-2.
The Oxford Dictionary of English Etymology, 1983 reprint. ISBN 0-19-861112-9.
Pappas, Theoni, The Joy Of Mathematics, Wide World Publishing; Revised edition (June 1989). ISBN 0-933174-65-9.
.
Peterson, Ivars, Mathematical Tourist, New and Updated Snapshots of Modern Mathematics, Owl Books, 2001, ISBN 0-8050-7159-8.
Marejeo mengine
Benson, Donald C., The Moment of Proof: Mathematical Epiphanies, Oxford University Press, USA; New Ed edition (December 14, 2000). ISBN 0-19-513919-4.
Boyer, Carl B., A History of Mathematics, Wiley; 2nd edition, revised by Uta C. Merzbach, (March 6, 1991). ISBN 0-471-54397-7.—A concise history of mathematics from the Concept of Number to contemporary Mathematics.
Davis, Philip J. and Hersh, Reuben, The Mathematical Experience. Mariner Books; Reprint edition (January 14, 1999). ISBN 0-395-92968-7.
Gullberg, Jan, Mathematics – From the Birth of Numbers. W. W. Norton & Company; 1st edition (October 1997). ISBN 0-393-04002-X.
Hazewinkel, Michiel (ed.), Encyclopaedia of Mathematics. Kluwer Academic Publishers 2000. – A translated and expanded version of a Soviet mathematics encyclopedia, in ten (expensive) volumes, the most complete and authoritative work available. Also in paperback and on CD-ROM, and online.
Jourdain, Philip E. B., The Nature of Mathematics, in The World of Mathematics, James R. Newman, editor, Dover Publications, 2003, ISBN 0-486-43268-8.
Maier, Annaliese, At the Threshold of Exact Science: Selected Writings of Annaliese Maier on Late Medieval Natural Philosophy, edited by Steven Sargent, Philadelphia: University of Pennsylvania Press, 1982.
Viungo vya nje
Chama cha Hisabati Tanzania , Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Free Mathematics books Free Mathematics books collection.
Encyclopaedia of Mathematics online encyclopaedia from Springer, Graduate-level reference work with over 8,000 entries, illuminating nearly 50,000 notions in mathematics.
HyperMath site at Georgia State University
FreeScience Library The mathematics section of FreeScience library
Rusin, Dave: The Mathematical Atlas . A guided tour through the various branches of modern mathematics. (Can also be found at NIU.edu .)
Polyanin, Andrei: EqWorld: The World of Mathematical Equations. An online resource focusing on algebraic, ordinary differential, partial differential (mathematical physics), integral, and other mathematical equations.
Cain, George: Online Mathematics Textbooks available free online.
Tricki , Wiki-style site that is intended to develop into a large store of useful mathematical problem-solving techniques.
Mathematical Structures, list information about classes of mathematical structures.
Mathematician Biographies. The MacTutor History of Mathematics archive Extensive history and quotes from all famous mathematicians.
Metamath. A site and a language, that formalize mathematics from its foundations.
Nrich, a prize-winning site for students from age five from Cambridge University
Open Problem Garden, a wiki of open problems in mathematics
Planet Math. An online mathematics encyclopedia under construction, focusing on modern mathematics. Uses the Attribution-ShareAlike license, allowing article exchange with Wikipedia. Uses TeX markup.
Some mathematics applets, at MIT
Weisstein, Eric et al.: MathWorld: World of Mathematics. An online encyclopedia of mathematics.
Patrick Jones' Video Tutorials on Mathematics
Citizendium: Theory (mathematics).
du Sautoy, Marcus, A Brief History of Mathematics, BBC Radio 4 (2010).
MathOverflow A Q&A site for research-level mathematics
Math – Khan Academy
Teachoo Maths
National Museum of Mathematics, located in New York City
!
Sayansi |
692 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Sheng | Sheng | Sheng ni lugha ya mitaani nchini Kenya inayochanganya Kiswahili na Kiingereza pamoja na lugha mbalimbali za kienyeji kama vile Kikikuyu, Kijaluo n.k. Sanasana hutumiwa na vijana katika mji wa Nairobi. Hata hivyo lugha hii inasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanaitumia. Sheng inatumiwa kwenye mabasi, redio, muziki, na hata wakati mwingine kwenye bunge la Kenya.
Sheng ilianza kutumika mwanzoni mwa miaka ya 1970 katika kitongoji cha Eastlands katika jiji la Nairobi. Wanamuziki, hasa wa mtindo wa "rap" wamefanya lugha hii kujulikana na kuanza kukubalika. Wanamuziki kama vile Kalamashaka jua kali na Nonini wamekuwa wakiitumia sana kwenye nyimbo zao.
Ingawa misamiati mingi, muundo, na kanuni za Sheng zinatoka kwenye lugha ya Kiswahili, Sheng inatumia maneno ya Kiingereza na pia lugha za makabila nchini Kenya. Ingawa kuna watu wengi wanaoipenda na kuitetea Sheng, wako wengine, wakiwemo walimu wa lugha shuleni na vyuoni, wanaoipinga kwa maelezo kuwa inaharibu lugha ya Kiswahili na pia inahatarisha uwezo wa watoto na vijana kumudu Kiingereza na Kiswahili sanifu.
Baadhi ya maneno ya Sheng
manzi, slay queen mshi, dame, chikidee, chile, chick, mradi, mresh, msupa = msichana
fiti!, fiti sana! = mzuri, okay
Kanairo = Nairobi
sasa = habari yako (ya sasa, ya saa hizi)
chali, mhi, kijanaa, aguy, jamaa = mvulana
kitu zii sana = kitu kibaya
kucheki = kuangalia
kuenda tao = kuenda mjini
kukatia = kumwambia unayempenda maneno matamu ("flirting")
kujiskia, kufeel fly/poa, kuji-do (do = fanya) = kuwa na maringo
kupata ball = kupata mimba
kugonga wall, kugonga mawe = kujaribu kumwongelesha msichana lakini hataki kujihusisha nawe
kulapa mtu = kujidai kuwa humwoni mtu
tia ritho = kuangalia (literally: put to the eye); katika Kikuyu, jina 'ritho' lamaanisha 'jicho'.
kushona = kupata mimba. Mfano: Dame ameshona
kuchill = hali ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa
kusota = hali ya kuwa bila pesa ama hela (being broke)
kuhanya = kufanya mapenzi holelaholela
keroro, kamunyueso = mvinyo, pombe
kugotea = kusalimia
kuwa gauge = hali ya kuwa mlevi
mahaga = sehemu ya nyuma ya msichana, matako
ndae = gari
kutia ndani, kuishi = kula
kupewa = kunywa pombe
Karao, Daewoo, = polisi (Daewoo kutoka jina la gari linalotumiwa na polisi nchini Kenya)
mchoro = mpangilio wa kufanya kitu (plan)
mgondi = jambazi (thug)
juala, CD = kondomu
kutia zii = kuachana na kitu ambacho unafanya
kula vako = kuamini uwongo. Mfano: Alikula vako eti dame yangu ni mlami (He/she believed that I have a white girlfriend)
veve = miraa
kindugulu = bangi
quarantei = karantini
kujiaisolet= hali ya kuwa peke yako/kujitenga
kuwa single = bila mke
chapa na tarimbo/kemba/nyandua = kujamiana kimapenzi
radha/ngori = shida
risto = hadithi nichapie risto
vajoo = bikra
kamunyueso/wain =pombe
bazenga = mtaalamu mi ni bazenga wa kucheza bukla
motino/dogi = mbwa
fwaka, fegi = sigara
mushogi = gari la aina ya matatu
kristi = mnunuaji
njege, sange, mabeast = polisi
yeng' = mwanamke
chums, dooh, weng' = pesa
sooh = shilingi mia moja
finje = hamsini
ashu = kumi
mbao =ishirini
kutypa = kumbuka
bazu = mheshimiwa
kuchum, kukis = kubusu
Sa Good = Mungu
mosmos = polepole
chapchap = harakaharaka
Njege = polisi
Tanbihi
Marejeo
Abdulaziz, Mohamed H. and Ken Osinde. 1997. Sheng and Engsh: development of mixed codes among the urban youth in Kenya. International Journal of the Sociology of Language 125 (Sociolinguistic Issues in Sub-Saharan Africa), pp. 45–63.
Bosire, Mokaya. 2006. Hybrid languages: The case of Sheng. Selected Proceedings of the 36th Annual Conference on African Linguistics, ed. Olaoba F. Arasanyin and Michael A. Pemberton, 185-193. Somerville, MA: Cascadilla Proceedings Project.
Fee, D., & Moga, J. 1997. Sheng dictionary.Third edition. Nairobi: Ginseng Publishers.
Githinji, Peter. 2005. Sheng and variation: The construction and negotiation of layered identities. PhD dissertation, Michigan State University.
Githinji, Peter. 2006. Bazes and Their Shibboleths: Lexical Variation and Sheng Speakers’ Identity in Nairobi. Nordic Journal of African Studies 15(4): 443–472.
Githiora, Chege. 2002. Sheng: peer language, Swahili dialect or emerging Creole? Journal of African Cultural Studies Volume 15, Number 2, pp. 159–181.
Kang’ethe, Iraki. 2004. Cognitive Efficiency: The Sheng phenomenon in Kenya. Pragmatics 14(1): 55–68.
Kießling, Roland & Maarten Mous. 2004. Urban Youth Languages in Africa. Anthropological Linguistics 46(3): 303-341
Mazrui, Alamin. 1995. Slang and Codeswitching: The case of Sheng in Kenya. Afrikanistische Arbeitspapiere 42: 168–179.
Ogechi, Nathan Oyori. 2002. Trilingual Codeswitching in Kenya – Evidence from Ekegusii, Kiswahili, English and Sheng. Doctoral dissertation, Universität Hamburg.
Ogechi, Nathan. 2005. On Lexicalization in Sheng. Nordic Journal of African Studies 14(3): 334–355.
Samper, David. 2002. Talking Sheng: The role of a Hybrid Language in the Construction of Identity and Youth Culture in Nairobi Kenya. PhD Dissertation, University of Pennsylvania.
Spyropoulos, Mary. 1987. Sheng: some preliminary investigations into a recently emerged Nairobi street language. Journal of the Anthropological Society 18 (1): 125-136.
Viungo vya nje
Dikshonari ya sheng Tupitie ucheki ma words za sheng za tene na zile nira
Tasnifu kuhusu Sheng Talking Sheng: The role of a hybrid language in the construction of identity and youth culture in Nairobi, Kenya.
Kamusi ya Sheng/Kiingereza, Kiingereza/Sheng
Blogu ya Sheng Bloki ya Osporne
Lugha
Lugha za Kenya |
693 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiswahili | Kiswahili | Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (35%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.
Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.
Historia ya lugha
Lugha ilianza takribani miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu.
Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.
Kando ya Kiarabu toka zamani pia kuna athira ya lugha mbalimbali kama Kiajemi, Kihindi na Kireno.
Kuanzia karne ya 20 hadi sasa maneno mengi yamepokewa kutoka Kiingereza, na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kifaransa, lakini pia kutoka lugha nyingine, hasa Kiarabu.
Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawahili au لغة سواحيلية lugha sawahiliya).
Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa.
Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika.
Tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea barani kwa njia ya biashara.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza lugha ilisanifishwa na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye msingi wa lahaja ya Unguja.
Wasemaji
Hakuna hakika kuhusu idadi ya wasemaji wa lugha hiyo; idadi zinazotajwa zinatofautiana, lakini ni kati ya milioni 100 na 200 , kwa sababu wasemaji wanaoitumia kama lugha ya kwanza hawapungui milioni 20, na wasemaji wanaoitumia kama lugha ya pili ni zaidi ya milioni 90.
Tena idadi ya wasemaji wa lugha ya kwanza inakua haraka, kwa sababu lugha inaenea katika maeneo ambapo hapo awali lugha nyingine zilitawala; hasa katika miji ya Tanzania imekuwa lugha kuu, badala ya lugha za kikabila, kutokana na mchanganyiko wa watu hata ndani ya nyumba moja, kama vile wanapooana watu wa makabila tofauti, jambo ambalo limekuwa la kawaida hasa Tanzania, ambayo inaongoza kwa matumizi ya Kiswahili. Kwa watoto wengi kimekuwa lugha mama.
Kati ya nchi nyingine ambapo Kiswahili kinatumika kuna Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia, Zambia, Malawi na visiwa vya Bahari Hindi kama Visiwa vya Ngazija (Komoro).
Lugha rasmi
Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na katika nchi zifuatazo:
Tanzania: ni lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, makanisani, misikitini, redioni, kwenye runinga na idadi kubwa ya magazeti. Serikali inatakiwa kukiendeleza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa. Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu, ingawa utekelezaji wake umesimama.
Kenya: ni lugha ya taifa tena lugha rasmi, sawa na Kiingereza, baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Hata hivyo, lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila.
Uganda: kimetangazwa kuwa lugha ya taifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumiwa na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani. Wona UBC, WBS tv. Mwaka 2005 bunge lilipiga kura kukifanya lugha rasmi ya pili kwa kuwa kinazungumzwa zaidi (nje ya Buganda).
Rwanda: tarehe 8 Februari 2017 bunge lilifanya Kiswahili lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa (pamoja na Kilingala, Kiluba na Kikongo), pia lugha ya jeshi. Kiswahili kilifika mashariki ya nchi na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba.
Lugha ya kwanza, lugha ya pili
Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya.
Kimeenea zaidi kama lugha ya mawasiliano na biashara pale ambako watu wa makabila mbalimbali wanakutana. Pamoja na nchi zinazotajwa hapo juu Kiswahili kinatumika Kaskazini mwa Msumbiji, Kusini kabisa ya Somalia, Mashariki mwa Burundi.
Maeneo ya mpaka wa Tanzania kuna pia wasemaji kadhaa huko Malawi na Zambia.
Tanzania na Kenya zilipokea wakimbizi wengi waliojifunza Kiswahili lakini hakuna uhakika kama bado kinatumiwa nao baada ya kurudi Afrika Kusini, Rwanda, Sudan Kusini, Somalia n.k.
Kimataifa
Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Afrika ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni na wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika.
Leo imekuwa inatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbalimbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche Welle, Monte Carlo, RFI, na nchi nyinginezo kama vile Uchina, Urusi, Irani.
Aidha, imekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya bara, Urusi, Uchina, na barani Afrika.
Mwaka 2018 Afrika Kusini ilikubali Kiswahili iweze kufundisha shuleni kama somo la hiari kuanzia mwaka 2020. Botswana ilifuata mwaka 2020, na Namibia ina mpango kama huo. Pia Ethiopia na Sudan Kusini zimeanza kufundisha Kiswahili.
Maendeleo ya Kiswahili
Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.
Kuna mzaha unaosimuliwa hasa Tanzania: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kilikua Tanzania Bara, kikafa Kenya na kuzikwa Uganda. Hali halisi Kiswahili kina maendeleo yake katika nchi hizo zote labda zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo matumizi yake ni kwa njia ya lahaja za Kingwana.
Lakini itategemea pia juhudi za serikali kama umoja wa lugha utatunzwa kwa sababu kuna athari nyingi kutoka lugha za kila eneo zinazoingia katika ukuzi wa Kiswahili kwa namna zinazotofauitiana.
Taasisi zinazokuza Kiswahili
Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda.
Nchini Tanzania kuna Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) ilhali nchini Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA).
Uchunguzi wa Kiswahili huendelea pia katika idara za vyuo vikuu vingi duniani, kwa mfano katika Institute National des Langues et Civilisations Orientales, jijini Paris, Ufaransa.
Kamusi za Kiswahili
Kati ya shughuli muhimu za taasisi hizo, mojawapo ni kazi ya kukuza misamiati ya Kiswahili yaani kutafuta maneno mapya au kupanua matumizi ya maneno yaliyopo ili kutaja mambo ya maisha ya kisasa yaliyobadilika. Utunzi wa kamusi za Kiswahili hupanua elimu hiyo.
Faida za kutumia Kiswahili kwa mataifa ya Afrika
Faida za kutumia lugha ya Kiswahili zinatajwa kama ifuatavyo:
1. Husaidia kuleta umoja wa bara zima.
2. Hudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba.
3. Hufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.
4. Hurahisisha mawasiliano baina ya watu wa Afrika Mashariki.
5. Husaidia kuwa na mahusiano ya kibiashara na watu mbalimbali.
6. Ni ishara ya kuwa huru na kushikamana.
7. Ni utambulisho wa jamii husika (utaifa).
8. Husaidia kukuza na kuendeleza sanaa.
9. Husaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika taifa husika.
10. Husaidia kupata ajira katika vyuo na shule mbalimbali zinazofundisha lugha ya Kiswahili hata nje ya nchi.
11. Husaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wa lugha hiyo watakaofanya vizuri katika masomo kwa kuyaelewa zaidi.
12. Husaidia kuikuza na kuieneza ndani na nje ya jamii.
Mengineyo
Siku ya Kiswahili Duniani ilianzishwa na UNESCO mnamo mwaka 2021 ili kuadhimishwa kila tarehe 7 Julai kuanzia mwaka 2022.
Tazama pia
Historia ya Kiswahili
Uenezi wa Kiswahili
Lahaja za Kiswahili
Kamusi za Kiswahili
Tanbihi
Marejeo
Ashton, E. O. 1944. Swahili Grammar (Including Intonation). London: Longmans.
Hinnebusch, T. J. 1979. "Swahili". Katika: T. Shopen (mhariri) Languages and Their Status, uk. 209-293. Cambridge, Massachusetts: Winthrop.
Hinnebusch, T. J., and S. M. Mirza. 1979. Kiswahili: Msingi wa Kusema, Kusoma na Kuandika. Lanham, MD: University Press of America.
Shihabdin Chiraghdin et Mathias E. Mnyampala. Historia ya Kiswahili. Oxford University Press, 1977.
Nurse, D. and Hinnebusch, T. J. 1993. Swahili and Sabaki: A Linguistic History. Berkeley and Los Angeles: University of California Press.
Ohly, Rajmund, Warsaw: Wydawnictwa Uniwersytetu warszawskiego,
Język suahili,
Ⅰ. Zarys gramatyki ⅠⅠ. Wybór tekstów, 1969 ;
Ⅴ Teksty suahili w piśmie arabskim wraz z ćwiczeniami i wprowadzeniem metodologicznym, 1972,
Literatura suahili, 1972.
Ohly, R., Kraska-Szlenk, I., and Podobińska, Z., Język suahili, Warsaw: Wydawnictwo Akademickie Dialog, 1998.
Wald, B. 1987. "Swahili and the Bantu Languages". Katika: B. Comrie (mhariri) The World's Major Languages, uk. 991-1014. New York: Oxford University Press.
Whiteley, W. 1969. Swahili: The Rise of a National Language. London: Methuen.
Zawawi, S. 1971. Kiswahili Kwa Kitendo: An Introductory Course. New York: Harper & Row.
Viungo vya nje
makala za OLAC kuhusu Kiswahili
lugha ya Kiswahili katika Glottolog
http://www.ethnologue.com/language/swh
"Kiswahili, lugha moja ya Tanzania (Kiingereza)
Jifunze Kiswahili (Kiingereza)
Kamusi Hai ya Kiswahili/Kiingereza
Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza
Tovuti kwa Kiitaliano yenye maelezo mafupi kuhusu lugha ya Kiswahili, Kozi kwa mtandao na Kamusi ya Kiitaliano - Kiswahili
Mwana Simba: Kiswahili? Hakuna matata! (Kiingereza/Kifaransa)
Swahili Literatur/Fasihi ya Swahili (Kijerumani/Kiswahili)
Woerterbuch/Kamusi Kiswahili/Deutsch Deutsch/Kiswahili (Kijerumani/Kiswahili)
Vitabu vya Kiswahili na du Kijerumani / Swahili-Buecher und Übungen
Mafunzo ya Kiswahili kwa video
Afrika
Lugha za Burundi
Lugha za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Lugha za Kenya
Lugha za Rwanda
Lugha za Tanzania
Lugha za Uganda
Lugha za Kibantu
Waswahili
Jumuiya ya Afrika Mashariki |
882 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Mwanzo | Mwanzo | <center>
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
<small>
Idadi ya makala:
Idadi ya kurasa zote: (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Idadi ya hariri:
Idadi ya watumiaji waliojiandikisha:
Idadi ya wakabidhi:
Idadi ya watumiaji hai: (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
Takwimu ya WIkipedia ya Kiswahili kwa jumla
Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
hapa kwenye takwimu za makala
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia ( andika jina la mtumiaji kwenye sanduku)
Jumuia za WikimediaWikipedia kwa lugha nyingine
|
888 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiarabu | Kiarabu | Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.
Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.
Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.
Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.
Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.
Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.
Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.
Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).
Asili ya lugha ya Kiarabu
Kiarabu, pamoja na lugha ya Kiebrania (ya Uyahudi) na Kiaramu (ya Mashariki ya Kati) na Kiamhari (ya Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi vile vile ambazo zinatokana na asili hii, kama Kiashuri, Kifinisia, Kibabili na kadhalika. Baadhi ya hizi lugha zimekufa au kuwa na wazungumzaji wachache, na kwa hiyo umuhimu wake umekuwa si mkubwa kama ulivyo umuhimu wa lugha ya Kiarabu.
Aina za Kiarabu
Kuna aina tatu kubwa za lugha hii ya Kiarabu:
Kiarabu Fasihi ambacho kilikuwa kikitumika zama za Ujahili kabla ya kuja Uislamu, na kuendelea kutumika baada ya kuja Uislamu katika Qurani na Sunnah za Mtume Muhammad,
Kiarabu Mamboleo ambacho kinatumika katika maandishi na mazungumzo rasmi baina ya Waarabu wote kwa jumla, na
Kiarabu Lahaja ambacho kinatumika na watu maalumu katika sehemu fulani za nchi au vijiji, na ni lugha ya mahali tu, kama vile Kiyemeni au Kimasri au Kishami au Kimaghribi, na lugha hizi au lahaja hizi zinakuwa zinatofautiana sana baina yake katika misamiati na matumizi.
Kiarabu fasihi
Kiarabu ni lugha ya zamani sana (tarehe yake inarudi nyuma zaidi ya miaka 2000), nayo pamoja na lugha nyinginezo za Kisemiti zilikuwa zikitumika katika nchi za Mashariki ya Kati. Kiarabu Fasihi ilianza kuwa na nguvu zaidi baada ya kuteremshwa Qurani kwa lugha hiyo na kuhifadhiwa Hadithi za Mtume Muhammad na kuwa ndio chanzo cha lugha zote nyinginezo za Kiarabu zilizokuweko wakati huo.
Fasihi ya Kiarabu isiyo na tabia ya kidini ilikuwa hasa Ushairi. Washairi kama Abu Nuwas, Omar Khayyam, Hafiz, ibn Qayyim al-Jawziyyah wanakumbukwa hadi leo. Masimulizi kama Alfu Lela U Lela hayakuwa fasihi yenyewe, hata kama yamepata umaarufu katika nchi za Ulaya.
Maandishi mengine ya Kiarabu yaliyokuwa muhimu sana ni maandiko ya falsafa na sayansi. Waarabu walitafsiri maandiko ya Wagiriki wa Kale wakaendeleza ujuzi wao. Katika karne zilizopita Ulaya ilipokea sehemu kubwa ya elimu yake kutoka kwa Waarabu kwa njia hiyo.
Tangu karne ya 19 na katika karne ya 20 fasihi ya Kiarabu imepata uamsho mkuu. Khalil Jibran wa Lebanon yuko kati ya washairi wanaosomwa zaidi kimataifa. Nagib Mahfuz wa Misri ni mwandishi Mwarabu wa kwanza aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1988.
Tanbihi
Viungo vya nje
makala za OLAC kuhusu Kiarabu
lugha ya Kiarabu katika Glottolog
http://www.ethnologue.com/language/arb
Lugha za Kisemiti
Lugha za Algeria
Lugha za Iraq
Lugha za Libya
Lugha za Mauritania
Lugha za Misri
Lugha za Moroko
Lugha za Sudan
Lugha za Tunisia
Lugha za Syria
Lugha za Saudia
Lugha za Yemen
Lugha za Oman
Lugha za Falme za Kiarabu
Lugha za Katar
Lugha za Bahrain
Lugha za Kuwait
Lugha za Somalia
Lugha za Chad
Lugha za Israel
Lugha za Palestina
Lugha za Komori
Lugha za Gambia |
889 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad.
Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,800 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,400.
Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.
Imani na kitabu chake
Imani katika Uislamu ni kumwamini Mungu mmoja tu peke yake anayeitwa Allah, ambaye hajazaa wala hajazaliwa na hafanani na yeyote yule. Kitabu kitakatifu cha Waislam ni Qur'an ambayo inaaminiwa ilifunuliwa kwa Mtume Muhammad kutoka kwa Mwenyezi Mungu mbinguni kupitia malaika Jibrili; ni kawaida kusema Qurani "iliteremshwa" kwa Muhammad. Kwa imani hiyo, kabla yake walioteremshiwa kitabu ni Musa (Torati), Daudi (Zaburi) na Isa (Injili).
Pamoja na Qurani kuna mafundisho ya Sunna na Hadith ambayo ni maneno ya mtume Muhammad na masimulizi juu ya matendo yake ambayo pengine hutazamiwa kama mwongozo katika Uislamu.
Allah ndiye Mungu pekee na muumba wa kila kitu. Qurani inasisitiza kwamba hana mshirika, hana baba wala mwana, hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mwanzo wala mwisho.
Pamoja na amri mbalimbali kuna mfumo wa sheria za kidini zinazoitwa kwa jumla "sharia"; inajumlisha maagizo kuhusu mambo mengi ya maisha ya kila siku, uchumi na siasa.
Historia ya chanzo cha Uislamu
Muhammad alizaliwa mnamo mwaka 570 BK kama mtoto wa mfanyabiashara mjini Maka uliopo kwenye Bara Arabu.
Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu malaika Jibril alimtokea alipokuwa na umri wa miaka 40 yaani mnamo mwaka 610. Kutoka kwa malaika alipokea maneno ya Kurani na ufunuo huu uliendelea hadi mwisho wa maisha yake.
Mtume alitangaza yale aliyosikia kwa wafuasi wake na maneno haya yalianza kukusanywa tayari wakati wa maisha ya mtume. Baada ya kifo chake mwaka 632 khalifa wa tatu Uthman ibn Affan alikusanya muswada na kumbukumbu zote na kuziweka pamoja na kuwa kitabu kamili.
Ujumbe uliohubiriwa na Muhammad huko Maka ulipata wasikilizaji wachache, lakini viongozi wengi wa Kikuraishi, waliokuwa kabila kubwa Maka, waliwaona kama hatari kwa Maka na mwaka 622 Waislamu walipaswa kutoka Maka wakahamia Yathrib mji wa jirani uliojulikana baadaye kama Madina.
Uhamisho huu unaitwa hijra na tangu khalifa wa pili Umar ibn al-Khattab huhesabiwa kuwa ni chanzo cha kalenda ya Kiislamu.
Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye "madinat an-nabi"" ikajulikana kwa kifupi kama Madina.
Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuza Wayahudi wa Yathrib.
Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu liliingia mjini Maka.
Mtume alipoaga dunia mwaka 632 sehemu kubwa ya Bara Arabu ilikuwa chini ya Uislamu tayari.
Mafunzo ya Uislamu
Uislamu unawafunza wafuasi wake mambo mengi yanayohusiana na maisha, ikiwa yale yanayohusu ibada kama Sala, Zakat, Saumu na Hija; ambazo pamoja na kauli ya Shahada ("Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake") huitwa nguzo za Uislamu au yale yanayohusu maingiliano baina ya wanadamu, yakiwa maingiliano ya kijamii kama ndoa na talaka na ujirani mwema, au ya kiuchumi kama biashara, au ya kisiasa kama kawaida za kumchagua kiongozi wa dola, au ya uhusiano baina ya mataifa mbali mbali ulimwenguni.
Uislamu unatazamwa kuwa mfumo kamili wa maisha ya binadamu, kiimani, kimaisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Ibada katika Uislamu
Ibada katika Uislamu ni vile vitendo ambavyo Muislamu anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, kwani ibada yoyote haitakikani iwe na ushirikina ndani yake, na wakati itakapokuweko aina yoyote ya shirki basi ibada ile inakuwa haina maana wala thawabu wala ujira wowote, ni kazi ya bure.
Kwa hiyo, kila Muislamu anatakikana wakati anapofanya ibada yake afanye kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba akampa kila aina ya neema na kumtukuza kuliko viumbe vingine vyovyote, kwa kumpa akili, fahamu na elimu.Nguzo zauislamu :(Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Nguzo tano za Uislamu
Kuna matendo kadhaa ambazo zinaitwa "Nguzo za Uislamu". Kwa kawaida ni tano zinazofundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.
Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi kwa nguzo tano halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano .
Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.
Salat: (Kiarabu: صلاة) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
Zakat: (Kiarabu: زكاة) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.
Maingiliano katika Uislamu
Uislamu umeweka kawaida mbali mbali katika maisha wakati watu wanataka kuweka uhusiano fulani baina yao ili mambo yaende vizuri na uhusiano uzidi kuwa mwema baina yao. Katika maingiliano yaliyowekewa kawaida na nidhamu katika Uislamu ni mambo yanayohusu:
Nikaha au ndoa baina ya Waislamu
Biashara na mambo yanayohusu uchumi
Uhusiano wa kijamii baina ya watu katika mtaa au kijiji au mji au nchi
Uhusiano wa kimataifa baina ya madola mbali mbali, yakiwa ya kiislamu au yasiyokuwa ya kiislamu.
Vikundi na madhehebu
Kuna mielekeo mikubwa miwili ndani ya Uislamu ambayo ni vikundi vya Wasunni 85-90% na Washia 10-15%.
Kundi kubwa ni Wasunni waliopata jina kutokana na Sunna ("kawaida") ya mtume; takriban asilimia 85-90 ya Waislamu wote huhesabiwa humo. Kati yao kuna madhehebu 4 ambao ni Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafii. Tofauti katika mafundisho si kubwa, zinahusu hasa sharia na fikh.
Kundi dogo zaidi ni Washia ambao wamegawanyika kati yao katika vikundi vingi. Washia walijitenga na Wasunni baada ya makhalifa wanne wa kwanza kuhusu swali ni nani anayefaa kuongoza Waislamu. Washia ni wale waliosisitiza sharti awe mtu kutoka ukoo wa Muhammad kupitia binti yake Fatima. Vikundi vya Washia vinatofautiana juu ya viongozi hawa. Jumuiya kubwa ya Washia ni Ithnashara walio wengi huko Uajemi, Irak na Lebanoni.
Viungo vya nje
Qurani Tukufu - Qurani Tukufu
http://www.islamhouse.com
tovuti ya Uislam - Mawaidha
Alhidaaya - Tovuti ya Kiislamu
Makasisi Waingia Uislamu
Mazungumzo ya Mwislamu na Mkristo |
890 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinaaminiwa na Waislamu kuwa ni "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hicho kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.
Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"
Kurani imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,445.
Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran na Waislamu, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile si ya Qur'an tukufu wala si ya kweli; ni nakala ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli.
Waarabu wa kabla ya Uislamu waliunda hadithi na hadithi juu ya miti, visima na milima, na waliunda ibada zinazohusiana na miamba na milima huko Safa, Marwa, Abu Kubeys, Arafat, Mina na Muzdalifah. Ingawa Qur'ani ilifuta ibada nyingine, haikupingana na maandiko ya Kiarabu yenye mizizi, badala yake, iliendeleza sana ibada hizo. Wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa Qur'ani bila kujua mazoea ya zamani; kihistoria, wanadamu hawakutumia kipimo cha wakati kikubwa kuliko mwezi. Hivyo, mtu ambaye alisema, "Nina umri wa miaka 200." alikuwa akihesabu miezi, sio miaka. Kwa kweli alikuwa na umri wa miaka 16. "Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa kati yao kwa miaka elfu, isipokuwa miaka hamsini." (Ankebut: 14)
Kwa kuongezea vyanzo vilivyoandikwa, masomo mengi na mashujaa, ambayo mengine ni tu katika utamaduni wa hadithi za Kiarabu, yamefunikwa kwa kifupi katika lugha ya Kurani, na marejeo madogo yanafanywa. Hadithi za Yusuf na Züleyha, İsa, Musa, İskender / Zülkarneyn ni hadithi ndefu zaidi. Hadithi za uumbaji na mafuriko, ibada ya Ibrahimu na Dhabihu, hadithi za manabii wa Kiebrania, imani ya Kiyahudi na historia, kama vile kutoka kwa Waisraeli kutoka Misri, zinachukua nafasi kubwa katika Kurani.
Historia
Waislamu wanaamini kwamba Qur'an mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti yake ilipomfikia.
Qur'an haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani.
Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu.
Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu.
Elementi, Sura, Mistari, Aya
Kuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari.
Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina.
Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan.
Mahusiano baina ya Qur'an na Biblia
Katika Qu'ran , inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizo pamoja na Uislamu huitwa Dini za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano hayo.
Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abrahamu, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Ayubu, Zekaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu.
Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu.
Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo.
Kurani na ulimwengu wa leo
Sheria zinazotegemea matamshi na ufafanuzi wa Kurani ni shida leo kuzilinganisha na haki za binadamu, usawa wa kijinsia na dini ya binafsi na uhuru wa kusema.
Tazama pia
Historia ya uandishi wa Qurani
Tanbihi
Marejeo
Al-Quran (Qurani) online kwa Kiarabu na tafsiri zaidi ya 100 katika lugha 20 pamoja na Kiswahili
Quran.com
Swahili Quran Tasfir by Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy,
Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Misahafu
Uislamu |
891 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi chake cha utume. Hadithi hizi ni mmoja kati ya miongozo ya imani kwa Waislamu.
Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona au kuyasikia katika muda wa utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali.
Asili
Muhammad aliishi miaka kama arobaini bila kuwa na imani ya Mungu pekee.
Kisha Mwenyezi Mungu akamletea mjumbe kutoka kwake aitwaye malaika Jibrili anayeaminiwa na Waislamu kuwa ndiye aliyempa aya zilizoko katika msahafu wa Waislamu, Kurani.
Inaelezwa kuwa Jibrili alimpa Muhammad aya hizo kwa muda wa miaka ishirini na mitatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.
Hadithi za Mtume Muhammad zimekusanywa katika vitabu vingi sana na wanazuoni mbalimbali wa Hadithi, lakini vitabu vya hadithi ambavyo ni muhimu na vinategemewa na wengi katika Uislamu ni hivi vifuatavyo:
Vitabu vya Hadithi
1- Sahih Al-Bukhari
2- Sahih Muslim
3- Sunan An-Nasai
4- Sunan At-Tirmidhi
5- Sunan Ibn Majah
6- Sunan Abu Daud
7- Muwatt'a Ibn Maalik
8- Musnad Ahmad bin Hanbal
Mtume Muhammad alikuwa hapendelei Hadithi zake ziandikwe wakati mmoja na Kurani, yasije yakachanganyika maneno yake na yale ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Hadithi zilichelewa kuandikwa mpaka baada ya kufariki kwake dunia kwa muda mkubwa kidogo, na kwa sababu hiyo Hadithi zikatawanyika sehemu mbalimbali kulingana na usahihi wake au udhaifu wake au uwongo wake.
Hivyo kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi: Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo).
Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama vile: kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi lenyewe na msimulizi wake.
Hadithi kwa mujibu wa fahamu na kutegemewa kwa msimulizi
Hadithi Sahihi huwa imesimuliwa kutegemewa ukweli wake na dini yake na mtu ambaye anafahamu nini anasimulia, na kuieleza hadithi kama alivyoipokea kutoka kwa Mtume Muhammad.
Hadithi Hasan au Nzuri huwa inajulikana asili yake na wasimulizi ni watu maarufu.
Hadithi Dhaifu huwa ile isiyofikia daraja ya Hasan, kwa sababu ya upungufu wa mmoja katika wasimulizi, au mfululizo wa wasimulizi haufikii mpaka kwa Mtume unakatika kwa mojawapo ya Masahaba, au mmoja katika wasimulizi si wa kutegemewa, na kuna kasoro fulani katika mambo haya.
Hadithi Maudhu'u (ya Uwongo) ni ile hadithi iliyobuniwa ikatiwa katika Hadithi za Mtume, na huwa kawaida inakwenda kinyume na Qurani au Hadithi nyinginezo Sahihi au Hasan, au kutonasibiana na maneno yake Mtume au kuwa msimulizi wa Hadithi hii ni mwongo, au kuwa msimulizi hakukutana na yule ambaye amesema amepokea kwake katika mfululizo wa wasimulizi waliotajwa, au kuweko kasoro fulani katika maelezo au matukio yaliyotajwa ndani ya Hadithi hio.
Hadithi kwa mujibu wa wasimulizi
Hadithi Qudsi ni ile hadithi ambayo Mtume Muhammad ameisimulia kutoka kwa Mola wake
Hadithi Marfu'u ni hadithi iliyopokewa na mfululizo wa wasimulizi na kufikishwa mpaka kwa Mtume
Hadithi Mauquf ni ile hadithi iliyosimuliwa na masahaba lakini wasiseme kuwa wameipokea kutoka kwa Mtume mwenyewe.
Hadithi Maqtu'u ni ile hadithi iliyokatika silsila au mfululizo wake .
Viungo vya nje
http://www.hadiths.eu
Uislamu
Misahafu |
End of preview. Expand
in Dataset Viewer.
README.md exists but content is empty.
Use the Edit dataset card button to edit it.
- Downloads last month
- 36