text
stringlengths
3
16.2k
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WIZARA ya Afya imesema ajali nyingi za barabarani nyakati hizi za sherehe, huchangiwa na matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Kwenye taarifa, Katibu wa Idara ya Afya ya Umma Mary Muthoni amesema kuwa miongoni mwa athari za matumizi wa dawa hizo ni kupoteza makini kwa madereva na hivyo kusababisha ajali. “Kukosa umakini, kukosa udhibiti wa gari na kuzubaa kutokana na matumizi ya mihadarati kwa kiwango kikubwa, ndivyo huchangia ajali za barabarani,” akaeleza. Bi Muthoni alitoa wito kwa madereva na Wakenya kwa ujumla kutoa kipaumbele kwa usalama wao na watu wengine katika jamii na wakome kutumia dawa za kulevya. Alisema miongoni mwa dawa zinazotumiwa vibaya ni nikotini na bangi. “Matumizi ya dawa za kulevya pia husababisha matatizo ya kimwili na kiafya na hata vifo,” akaonya Bi Muthoni. Hasara inayotokana na matumizi ya dawa za kulevya, Katibu huyo akaongeza, ni kwamba zinachangia kupungua kwa uzalishaji na hivyo kudumaza maendeleo ya kiuchumi na kijamii. “Ipo haja kwetu sote kushughulikia hatari za kiafya, kiuchumi na kijamii zinazohusiana na matumizi ya dawa hizi za kulevya kando na kuchangia ongezeko la ajali za barabarani na matatizo ya kiakili,” Bi Muthoni akasema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

LABAAN SHABAAN Na MASHIRIKA WAZIRI wa Fedha Profesa Njuguna Ndung’u amefichua kwamba serikali imelipa dola 68.7 milioni, sawa na Sh10 bilioni, za riba ya mkopo wa Eurobond. Ufichuzi huu kupitia kwa taarifa aliyotuma Prof Ndung’u unajiri siku chache baada ya kuibuka kwamba Ethiopia iliingia katika orodha ya mataifa matatu barani Afrika ambayo yamelemewa kulipa deni la kimataifa la kufadhili shughuli za serikali, Eurobond. “Tangu Julai 2023, serikali inaendelea kutekeleza mpango madhubuti wa ulipaji wa madeni ambao unahusisha kiasi cha mapato na mpango wa makubaliano nafuu ya ulipaji huo,” amesema Prof Ndung’u. Hii ni baada ya Ethiopia kukosa kulipa sehemu ya deni ambayo ni kuponi ya dola 33 milioni. Mapema mwezi wa Desemba 2023, nchi hii ya pili kwa idadi ya watu barani, ilitangaza imeshindwa kulipa deni la Eurobond. Chanzo cha hatua hii ni kwamba Ethiopia ilipigwa na dhoruba kali ya kifedha katika kipindi cha mlipuko wa Covid-19 na vita vya kijamii vya miaka miwili vilivyofika kikomo mnamo Novemba 2022. Taifa hilo lilihitajiwa kulipa sehemu ya deni Desemba 11, 2023. Lakini kwa sababu ya ‘kipindi cha neema’ cha majuma mawili, Ethiopia ilikuwa na mwanya hadi Desemba 26, 2023 kulipa kuponi ya dola 33 milioni. Haya ni kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa sahihi wakati wa nchi hiyo ilikabidhiwa deni la dola 1 bilioni. Kulingana na vyanzo viwili wa habari vilivyo na ufahamu wa mpango huu, wakopeshaji hawakuwa wamelipwa kufikia mwisho wa Ijumaa Desemba 22, 2023. Ijumaa ilikuwa siku ya mwisho ya benki ya kimataifa kufanya kazi kabla ya kipindi cha neema kukamilika. Serikali ya Ethiopia haikujibu maswali ilipohitajika kutoa maelezo ya hali Ijumaa na nyakati za wikendi. Kulemewa huku kwa taifa hilo kulitarajiwa kote na litajiunga na mataifa mengine mawili ya Afrika, Zambia na Ghana, katika kujipanga kikamilifu kwa ‘Mfumo wa pamoja.’ Kabla ya kufikia hapa, Ethiopia iliomba afueni ya deni chini ya mpango unaoongozwa na G20 mapema 2021. Maendeleo ya mpango huu yalicheleweshwa na vita vya kijamii wakati akiba ya fedha za kigeni ilididimia na mfumuko wa bei kuchupa. Wakati huo, wakopeshaji rasmi wa serikali ya Ethiopia, wakiwemo China, waliingia katika makubaliano ya kuahirisha huduma ya madeni Novemba 2023. Kufikia Desemba 8, 2023, serikali ilisema maelewano mbalimbali ambayo ilikuwa nayo na hazina za pensheni na wakopeshaji wengine wa sekta ya kibinafsi yaliporomoka. Mnamo Desemba 15, 2023, shirika la kimataifa la kutathmini ufaafu wa kukopeshwa la S & P Global, liliorodhesha Ethiopia kuwa ni taifa ambalo limeshindwa kulipa deni hilo. Shirika hili lilikuwa na dhana kwamba nchi hiyo isingeweza kulipa kuponi ya dola 33 milioni. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO “ALHAMDULILLAH!” alitamka Akida Iddi Mohamed,29, dakika chache baada ya kushuka kutoka kwa meli ya Idara ya Walinzi wa Baharini (KCGS) ya MV Doria. Alilia, akaomba na kuMshukuru Mungu kwa kumuokoa kwenye Bahari Hindi ambako alikaa na wenzake wawili kwa siku 22 baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama. “Siamini niko hai. Alhamdulillah,” alisema. Bw Mohamed ni mmoja wa wavuvi watatu ambao waliokolewa na meli ya uvuvi ya China baada ya boti lao la kuvua samaki kuzama mnamo Novemba 30. Baba huyo wa watoto wawili na mke mmoja alisema anasubiri kwa hamu kujumuika na familia yake. “Nataka tu kwenda nyumbani. Ni kisa cha maajabu, sijui vile tuliweza kuokolewa hai kwenye maji makuu,” aliongeza alipokuwa akikimbizwa katika hospitali kuu ya Pwani kwa uchunguzi wa afya. Wengine waliookolewa ni Hans Baraka na Fahad Mohammed, ambao walikaribishwa humu nchini na viongozi wa idara mbalimbali zinazohusika na masuala ya ubaharia wakiongozwa na Waziri wa Uchumi wa Baharini, Bw Salim Mvurya, mjini Mombasa. Bw Mvurya alisema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho huku maafisa wa usalama baharini wakiendelea kusaka mwili wa mvuvi mwingine aliyepotea. “Wavuvi hao walipotea baharini kwa siku 22. Lakini waliokolewa wakiwa salama. Tumewapeleka hospitalini kwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuwaunganisha na familia zao huku tukisaka mwili wa mwenzao,” alisema waziri Mvurya akipongeza maafisa wa usalama wa baharini kwa juhudi zao za uokoaji. Bw Mvurya aliwasihi wavuvi baharini, ziwani na mitoni kuwa makini wanapoenda kuvua samaki. Hata hivyo, alisema wizara yake itaendelea na mradi wa kuhamasisha wavuvi kuhusu usalama. Mkurugenzi Mkuu wa Maafisa wa Huduma za Usalama Baharini Bw Bruno Shioso aliwahakikishia familia ya mvuvi ambaye anakisiwa kuwa aliaga dunia wanaendelea kutafuta mwili wake. Hata hivyo alisema ajali hiyo imeonyesha umuhimu wa ushirikiano wa kuhakikisha usalama baharini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA RICHARD MUNGUTI WASHUKIWA sita, akiwemo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wanaodaiwa kuuza dhahabu bandia, watasherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya gerezani baada ya kunyimwa dhamana na korti katika kashfa ya Sh2.85 bilioni. Hakimu mwandamizi Bi Wandia Nyamu aliamuru washukiwa hao waliokana mashtaka mawili ya kumlaghai mfanyabiashara kutoka Malaysia pesa hizo, wasalie gerezani hadi Januari 9, 2024. Walioshtakiwa ni Muke Wa Mansoni Didier (raia wa Congo), Wakenya Patrick Otieno Oduar, Brian Otieno Anyanga, Makfish Riogi Kabete, Ken Omondi Kimboi, na Joshua Odhiambo Engade. Wote walikabiliwa na shtaka la kula njama kumlaghai Halid Bin Mohammed Yaacob Sh2.85 bilioni wakidai walikuwa na kilo 500 za dhahabu ambazo wangelimuuzia. Washtakiwa hao pia walikabiliwa na shtaka la kujaribu kumwibia Bw Yaacob pesa hizo katika mtaa wa Kileleshwa Nairobi. Washtakiwa hao walitiwa nguvuni Jumatano na maafisa wa kutoka kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa raia wa Malaysia Halid Bin Mohammed Yaacob kwamba amliitishwa takriban Dola 19 milioni (ambazo ni sawa na Sh2.85 bilioni) na washtakiwa hao wakidai wangemuuzia kilo 500 za dhahabu. Upande wa mashtaka ulisema washtakiwa hao walianza njama hizo za kutaka kumlaghai Bw Yaacob kati ya Oktoba 19 na Desemba 27, 2023. Mnamo Desemba 27, 2023, washtakiwa hao walijaribu kumwibia Bw Yaacob Sh2.85 bilioni kwa kumwonyesha vipande vya dhahabu bandia iliyokuwa imewekwa ndani ya masanduku. Mahakama ilielezwa washtakiwa hao walijua wanamndanganya Bw Yaacob hawakuwa na dhahabu hiyo. Wakili Simon Mburu aliomba washtakiwa waachiliwe kwa dhamana lakini upande wa mashtaka ulipinga ombi hilo. Bi Wandia alikataa kusikiliza ombi hilo la dhamana na kuamuru washtakiwa hao wazuiliwe katika gereza la Industrial Area hadi Januari 9, 2024, watakapowasilisha upya ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MASHIRIKA GASTON Glock, mhandisi na bwanyenye aliyetengeneza bastola aina ya Glock 17, aliaga dunia Desemba 27, 2023, akiwa na umri wa miaka 94, shirika la habari la Austria la APA limesema. Mnamo mwaka 2021 jarida la Forbes lilikadiria ukwasi wake kuwa ni dola 1.1 bilioni za Marekani. Glock alipata umaarufu mnamo miaka ya themanini (1980s) wakati jeshi la Austria lilikuwa linatafuta teknolojia ya kisasa katika utengenezaji wa silaha. Bastola aina ya Glock ilishabikiwa na wengi ambapo hata wanajeshi wa Marekani walianza kuitumia, huku pia ikisifiwa na wanamuziki akiwemo Snoop Dog. Mnamo mwaka 2003, wanajeshi wa Marekani walimpata Rais wa Iraq Saddam Hussein akiwa amejificha kwa shimo huku akiwa amejihami kwa bunduki aina ya Glock. Gazeti la the New York Times linasema baadaye walimkabidhi aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush silaha hiyo. Ingawa hivyo, wanaharakati wa kushinikiza udhibiti wa bunduki walimlaumu Glock kwa kutengeneza silaha ambayo ni rahisi kufichwa na yenye uwezo wa kubeba risasi nyingi. Mnamo Novemba 2018, mwanajeshi wa zamani wa nevi akiwa amejihami kwa kile polisi nchini Marekani ilisema ni bastola ya aina ya Glock ya uwezo wa kaliba .45 aliua watu 12 katika baa moja iliyoko Thousand Oaks, California. Mwanaharakati wa kushabikia wazungu, Dylann Roof, alitumia bastola aina ya Glock kuwaua watu tisa wa asili ya Waamerika-Weusi wakati wa somo la Bibilia katika kanisa mojawapo kule Charleston, South Carolina, mnamo Juni 2015. Glock mwenyewe akiwa na umri wa miaka 70, mnamo Julai 1999, aliponea kwenye jaribio la kutaka kumuua wakati broka aliyekuwa akisimamia biashara zake alikomboa bondia mstaafu kumshambulia kwa nyundo ya plastiki, mahakama iliambiwa. Ni baada ya Glock kutilia shaka broka huyo namna alivyokuwa akisimamia biashara zake na ndipo akaamua kutua Luxembourg kumkabili, mawakili walisema. Kufuatia shambulio hilo, broka Charles Ewert, na mshambuliaji Jacques Pecheur, wote wawili walifungwa jela. Ndoa ya miaka 49 kati ya Glock na mkewe Helga Glock ilivunjika kwa talaka mwaka 2011. Baadaye alimuoa Kathrin, mrembo ambaye alikuwa mdogo kwa miaka 50. Glock alikuwa na makazi mbele ya ziwa na yalikuwa na kituo cha vifaa vya kisasa vya michezo katika mkoa wa Carinthia, mandhari hayo yakiwavutia watu maarufu waliofika hapo kwa burudani na sherehe. Glock ameacha nyuma mkewe, binti na vijana wawili wa kiume. Mwenzake, Mikhail Timofeyevich Kalashnikov aliyezindua AK-47, ambayo ndiyo bunduki inayotumika sana duniani, naye alifariki mnamo Desemba 23, 2013, akiwa na umri wa miaka 94. AK-47 inatokana na jina la Avtomat Kalashnikova, lugha ya Kirusi kumaanisha “automatic Kalashnikov,” kutokana na jina la mvumbuzi huyo ambaye silaha hiyo yake iliidhinishwa mwaka 1947. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BENSON MATHEKA JUHUDI za jaji wa zamani wa Mahakama Kuu Said Chitembwe kuokoa kazi yake zimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali rufaa yake, ikisema kuna ushahidi alihusika na ufisadi. Jaji Chitembwe alipinga pendekezo la kuondolewa kwake afisini baada ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko kutoa kanda za video na rekodi za simu za rununu zikimhusisha jaji huyo na ufisadi. Mahakama ya Juu ilisema ushahidi uliotolewa mbele ya jopo iliyoteuliwa kumchunguza ulithibitisha kuwa mwenendo wake ulikiuka Kanuni za Maadili ya Tume ya Huduma ya Mahakama na pia ulikuwa kinyume na Ibara ya 168(1) (b) na (e) ya Katiba. “Mapendekezo ya jopo lililomchunguza kwa rais kwamba mlalamishi aondolewe kazini yanathibitishwa,” ulisema uamuzi wa majaji Mohamed Ibrahim, Smokin Wanjala na Njoki Ndung’u wa Mahakama ya Juu. Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta alimsimamisha kazi Jaji Chitembwe mnamo Mei 19, 2022, na kuunda jopo la mahakama ya watu saba kuchunguza madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya Jaji Chitembwe. Jopo hilo lililoongozwa na Jaji Mumbi Ngugi na wanachama wake walikuwa ni Wakili Mkuu Fred Ojiambo, Jaji Abida Ali Aroni, Jaji Nzioki wa Makau, James Ochieng’ Oduol, Luteni Jenerali (Mstaafu) Jackson Ndung’u na Lydia Nzomo. Mahakama hiyo ilianza vikao vyake mnamo Septemba 19, 2022, na kuwasilisha matokeo yake kwa Rais William Ruto baada ya kukamilisha uchunguzi wake mnamo Februari 7, 2023. Ilipendekeza kuwa Chitembwe hakufaa kuendelea kuwa jaji na kumtaka Rais William Ruto kumtimua kazini. Mwenyekiti jopo, Jaji Mumbi Ngugi alisema ilimpata jaji huyo na hatia ya utovu wa nidhamu. “Jopo, kwa kauli moja, ilipata jaji Chitembwe alikiuka Katiba akitekeleza majukumu yake,” alisema Jaji Ngugi. Rais Ruto aliishukuru jopo hiyo kwa kuharakisha kazi yake, na kusisitiza kuwa uongozi unahitaji uwajibikaji. Rais alisema wote wanaotwikwa jukumu la kuhudumia Wakenya wanapaswa kuongozwa na Katiba. ‘Ningetaka kuwakumbusha Wakenya kwamba kuna mbinu za kushughulikia hali yoyote ambapo mtu anashukiwa kutenda kinyume na sheria akitekeleza majukumu ya umma,’ alisema Rais Ruto. Rais aliahidi kushughulikia mapendekezo ya jopo hilo. “Nitafanya kile ambacho Katiba inatarajia kutoka kwangu,” alisema Rais. Jopo lilimpata na hatia ya ya kujadili kuondolewa kwa kesi katika Mahakama ya Rufaa huko Malindi katika makazi yake huko Mountain View, Waiyaki Way Nairobi. Alijadili suala hilo na Jane Mutulu Kyengo, Mike Sonko, Jimmy Askar, Amana Saidi Jirani miongoni mwa wengine. Kesi hiyo ilikuwa kati ya Pacific Frontiers Seas Limited na Bi Kyengo. “Jaji alijifanya makosa kwa kushauri pande zote utaratibu unaopaswa kufuatwa kukata rufaa ambayo iliwasilishwa dhidi ya hukumu yake mwenyewe na kuahidi kujadili suala hilo na majaji wengine na maafisa wa mahakama waliokuwa wakishughulikia rufaa hiyo,” jopo lilisema. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WANDERI KAMAU KATIKA wakati huu mgumu ambao Wakenya wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na gharama ya juu ya maisha, serikali ya Kenya Kwanza inashikilia kuwa sera za kiuchumi za Rais William Ruto zimeiokoa nchi pakubwa. Jumatano, Desemba 27, 2023, Msemaji wa Serikali, Bw Isaac Mwaura, alisifia sera za kiuchumi za Rais Ruto, akisema kwamba zimeifaidi Kenya pakubwa. Kupitia ujumbe alioweka kwenye mtandao wa ‘X’ (zamani ukijulikana kama Twitter), Dkt Mwaura alisema kuwa sera ambazo Rais Ruto ametekeleza tangu kuchukua uongozi, zimeiepusha Kenya kuingia katika mgogoro mkubwa wa kushindwa kulipa madeni yake. Alisema ni hali ambayo mataifa mengine barani Afrika na duniani kote yamejipata. Licha ya baadhi ya sera kutoonekana kuwa maarufu miongoni mwa raia, Bw Mwaura alisisitiza kuwa zinaipeleka Kenya katika mwelekeo mzuri. “Rais William Ruto amefanya maamuzi magumu japo yatakayoikoa nchi yetu dhidi ya kutumbukia kwenye ugumu wa kushindwa kulipa madeni yake. Watu wengi walifikiri kwamba huenda tukashindwa kulipa madeni yetu. Hata hivyo, hilo halikufanyika,” akasema Bw Mwaura. Alisema kuwa Rais Ruto aliweka maslahi ya nchi mbele, hivyo wale ambao wamekuwa wakimkosoa wataona manufaa ya maamuzi hayo. “Wakati mwingine, baadhi ya maamuzi tunayoyafanya huenda yakawa magumu. Hata hivyo, nyakati zitakavyosonga, hata wakosoaji wetu huanza kukubaliana nasi,” akasema Bw Mwaura. Kauli yake ilijiri siku chache baada ya ripoti kuibuka kwamba Ethiopia imeshindwa kulipa mkopo wake wa Eurobond, hilo likiifanya nchi ya tatu kushindwa kulipa mkopo wake. Mataifa mengine ambayo yameshindwa kulipa mikopo yake ni Zambia na Ghana. Kulingana na ripoti zilizochapishwa na mashirika kadhaa ya habari ya kimataifa, Ethiopia ilisema itashindwa kulipa mkopo wake kutokana na changamoto za kiuchumi ambazo imekuwa ikipitia kutokana na athari za janga la virusi vya Covid-19. Vita vya miaka miwili ambavyo vilikumba nchi hiyo pia imetajwa kuchangia ugumu wake kushindwa kulipa mkopo huo. Vita hivyo baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kundi la Tigray Peoples’ Liberation Front (TPLF) vilikamilika Novemba 2022,  chini ya mazungumzo yaliyoendeshwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. Kwenye kikao na wanahabari wiki iliyopita, Rais Ruto alisema alilazimika kuchukua hatua kali ili kuiepusha Kenya kushindwa kulipa mikopo yake inayodaiwa na taasisi za kifedha kama vile Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia, mataifa kama China kati ya mengine. “Uchumi wetu sasa ni thabiti na huo ndio ukweli. Ikiwa singechukua uongozi wa taifa hili, ukweli ni kuwa tungetumbukia kwenye shimo la kushindwa kulipa madeni yetu kama baadhi ya nchi barani Afrika. Najua maamuzi hayo ni magumu, japo ni afadhali kuyafanya wakati huu, badala ya kungoja na kuona taifa hili likishindwa kulipa madeni yake,” akasema.
Tags
You can share this post!
Previous article
Lalama za ongezeko la walemavu Pokot Magharibi 
Next article
Mahakama yazima juhudi za Chitembwe kurudi
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na...
Malkia wetu leo ni  Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu...
Sayfer Godez ni mkaazi wa Nakuru .Anapenda kushiriki kwenye majukwaa ya mapambo na urembo.Uraibu wake ni kusafiri na kujumuika na... Sylvia Wangeci 23 ni mzaliwa wa Molo, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu Cha MKU tawi la Nakuru.Uraibu wake ni kusafiri na... Mical Abulatsia Imbukwa, 28, ni mwanahabari katika shirika moja jijini Nairobi. Uraibu wake ni kutazama filamu za Afro sinema na kujumuika... Faith Karungari mwenye umri wa miaka 22 ni mwanafasheni na mwanamitindo maarufu kutoka Nakuru.Uraibu wake ni kuogelea na kusikiliza muziki... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ya Juu jana ilianza kusikiza rufaa ya mpango wa kubadilisha katiba (BBI) huku Mwanasheria Mkuu Bw Paul... Na BENSON MATHEKA
RAIS Uhuru Kenyatta jana Jumapili alisema kuwa ndoto yake ya kubadilisha katiba ya Kenya iliyopitishwa 2010 kupitia... Na CHARLES WASONGA
KWA mara nyingine Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa mageuzi ya katiba yaliyopendekezwa katika Mswada wa Mpango wa... Na JOSEPH WANGUI
Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa... Na Gitonga Marete
KIONGOZI wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi amesisitiza kuwa Bunge linapaswa kurejelea Mpango... Na Leonard Onyango
NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua... Na CHARLES WASONGA
JUHUDI za wabunge wanaoegemea mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kutumia bunge kupitisha... Na WALTER MENYA
JUHUDI za kuokoa mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI) zimefikishwa rasmi katika Mahakama... Na FRANCIS MUREITHI
KUSAMBARATIKA kwa Mpango wa Kubadilisha Katiba (BBI) kumefifisha pakubwa ushawishi wa kisiasa wa mwenyekiti wa Kanu,... Na WANDERI KAMAU
README.md exists but content is empty.
Downloads last month
33